security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
Kwa kilichotokea leo ni wazi kuwa CHADEMA hawajajiandaa, hawakujipanga, hawakufanya maandalizi na wala hawana matarajio na matumaini ya ushindi, wameanza wakiwa wamekata tamaa na wametangaza kushindwa kabla ya kuanza kushindana. Ukiwapima na ukipima mkutano wao katika maeneo yafuatayo utakubaliana na nilichokiandika.
1: Mkutano ulikosa maandalizi, kuanzia watu wa hamasa mpaka wazungumzaji.
Kila aliyesimama kuzungumza alionyesha wazi kabisa kuwa hakuwa amejipanga kuzungumza katika mkutano mkubwa kama huo wa ufunguzi ambao kimsingi ndio unatambulisha agenda ya Chama kwa wanachama na wananchi kwa ujumla wao.
Kawaida ya siasa za Chadema hutanguliwa na hamasa kubwa katika mitandao ya kijamii, mtaani na katika eneo husika la mkutano. Maeneo yote hayo hakukuwa na hamasa ya aina yeyote.
2: Idadi ndogo ya wanachama waliojitokeza kuhudhuria.
Labda kutokana na kukosekana kwa hamasa watu wachache sana walijitokeza katika viwanja hivyo ambapo imeonyesha kuwa kama vile watu wameupuuzia mkutano huo.
3: Siku ya Mkutano na eneo la Mkutano
Mbagala ni eneo la wakazi waislamu na kwa siku ya ijumaa kwa waislam inajulikana kuwa wameitenga siku hiyo kwasababu ni siku yao ya ibada na kwamba wanajipa mapumziko yasiyo rasmi katika kazi na shughuli zao. Wlaikosea kupanga mkutano huo kwa siku hii ya leo na eneo hilo.
4: Nafasi ya vyombo vya habari,
Chadema wameneglect kabisa umuhimu wa vyombo vya habari katika kulifanyia branding tukio lao na kulipa vibe ambayo ilitegemewa, matokeo yake Mwenyekiti ndio kaharibu zaidi baada ya kuituhumu TBC kuwa imekata matangazo.
5: Hotuba ya Mgombea
Katika siku kubwa kama ya uzinduzi hautakiwi kuzungumza vitu obvious, ni siku ya kuieleza dunia nini CHADEMA imepanga kufanya sio siku ya kuja kusimulia matukio ambayo kwa miaka mitatu watu wamekuwa wakiyasikiliza.
6: Wahuni ambao walikuwa wamekaa mbele wanapiga mayowe na kumfanya Mgombea akate hotuba na kuanza kuwaengage ili watulie na kuanza kuzungumza nao.
7: Nafasi ya wasanii na watu wa kutoa hamasa;
hakukuwa na msanii yeyote wa maana ambapo kwa mbagala wangeweza kutafuta waimba singeli hata watatu tu wangetosha kuongeza idadi ya watu na kuupa mkutano vibe linalostahili.
8: Kuutumia Mkutano wa Ufunguzi kama sehemu ya tukio la fundraising;
Ni ujinga uliopindukia kuutumia mkutano ule kufanya fundrising badala ya kunadi sera, wakati huo kwa miaka mitano MWENYEKITI amekuwa akikusanya hela ya wabunge kwa kile alichokiita Mfuko wa Uchaguzi.