CCM Wauwana - Visu, risasi vyatumika

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Kitimtim cha kura za maoni kwa ajili ya kupitisha wagombea wa CCM kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Oktoba mwaka huu kimezua maafa wilayani hapa baada ya kada mmoja maarufu kuuawa huku mwingine akinusurika kimiujiza kutokana risasi kadhaa zilizomwagwa nje nje.

Matukio hayo ya kusikitisha, yametokea hivi karibuni katika maeneo ya vijiji vya Nyambureti na Itururu, ambapo kada aliyeuawa ametajwa kwa jina la Justin Mkami almaarufu kama Msangi, mwenye umri wa miaka 41.

Taarifa za kifo cha kada huyo wa CCM na ambazo zimethibitishwa leo asubuhi na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Liberatus Barlow, zinasema marehemu ameuawa baada ya kuchomwa visu na kisha utumbo wake kutoka nje.

Inaelezwa zaidi kuwa alifia katika Hospitali Teule ya Nyerere wilayani Serengeti ambako alikimbiziwa baada ya kuchomwa kisu wakati wa kampeni na mtu anayetajwa kwa jina la Hiriza Mairo.

"Ni kweli kuna tukio kama hilo la mauaji linalohusiana na mambo ya chaguzi za siasa... na mtuhumiwa wa mauaji hayo aitwaye Mairo amekimbia na anaendelea kusakwa na polisi," akasema Kamanda Barlow.

Akieleza zaidi, Kamanda Barlow amesema kuwa marehemu Justin alikutwa na mkasa huo wakati akiwa kwenye kampeni za mmoja wa wanaowania nafasi ya ugombea wa Mwenyekiti wa Kijiji.
Akasema wakati akiendelea kumpigia debe mmoja wa wagombea hao, ndipo mtuhumiwa anadaiwa kumvaa na kumchoma visu vya tumboni, kitendo ambacho kilimsababishia umauti.

"Uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hili unaendelea," akasema Kamanda Barlow.

Aidha, Kamanda Barlow amesema kuwa katika tukio jingine linalohusiana na kura za maoni, Bw. Jospiter Karere, 48, Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Itururu, Tarafa ya Ikorongo wilayani Serengeti, amenusurika kuuawa baada ya risasi kadhaa kumwagwa.

Akasema Karere alikumbana na mkasa huo wakati wa kampeni za kuwasaka wanaowania nafasi ya kugombea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi Oktoba.

Hivi karibuni, vurugu pia ziliibuka katika kura za maoni Jijini Dar ambako wanachama kadhaa walijeruhiana na baadhi ya kadi za CCM kuchanwachanwa.

CHANZO: ALASIRI
 
hapo ni mwanzo tu bado NEC hawajaanza kuchinjana wakati wa ubunge na urais Yetu majicho
 
hapana hizi ni dalili za mabadiliko, msiogope, wa kufa watakufa lakini wapo watakao baki
 
Hii inaonyesha wana CCM walivyo na uchu wa madaraka.
Yetu macho, tusubiri tuone ya mwakani.
Eee Mungu tunusuru.
 
Sitashangaa kama ni Mkoa wa Mara ila 2010 tusubirie mengi zaidi ya haya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…