Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
Na Ally Sonda, Moshi
KATIKA hali inayoonekana kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekusudia kumng'oa Mbunge wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo (Chadema) ifikapo mwaka 2010, kimeamua kuutumia Umoja wa Vijana (UVCCM) katika kufanikisha ndoto hiyo.
Ombi hilo la kuitaka UV-CCM itumike katika harakati hizo lilitolewa jana na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Profesa Jumanne Maghembe wakati akifungua mkutano mkuu wa umoja huo mkoani hapa na kusisitiza kuwa jimbo hilo kuendelea kushikiliwa na upinzani ni aibu kwa CCM na jumuiya zake, ikiwemo ya vijana.
Bila kumtaja moja kwa moja Ndesamburo, Profesa Maghembe alisema CCM haina budi kuwatumia vijana wake mwaka 2010 ili kuing'oa Chadema, ambayo alidai inatamba kuwa haiwezi kung'olewa kwenye jimbo la Moshi Mjini.
"Vijana nawaombeni sana hakikisheni mnakisaidia chama kukiondoa hiki kibabu kinachong'ang'ania hapa Moshi Mjini, lazima mwaka 2010 CCM ipate ushindi hapa Moshi mjini," alisema Profesa Maghembe bila kumtaja Ndesamburo.
Akizungumzia uhai wa jumuiya ya vijana, Maghembe ambaye pia ni waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, aliwataka vijana kuwa wabunifu katika kuanzisha miradi ili waweze kujitegemea na kuacha tabia ya kuwa ombaomba.
Aliwataka vijana watumie muda wao mwingi kufanya kazi za uzalishaji na vilevile kuwaeleza wananchi mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyopatikana ndani ya utawala wa serikali ya CCM, ikiwemo ubora wa elimu kwa kuongeza idadi ya shule na vyuo vikuu.
"Vijana acheni tabia ya kukaa kimya wakati mnaona serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete inavyofanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo ya elimu, afya, mawasiliano, maji na michezo... lazima mfanye kazi ya kuwaeleza wananchi," alisema.
Kuhusu suala la ufisadi, Profesa Maghembe aliwataka vijana kuisaidia serikali ya Rais Kikwete ili iendelee kuwanasa na kuwaburuza mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi, wakiwemo wale walioitia nchi hasara ya mamilioni ya fedha kwa kutoa misamaha ya kodi.
"Vijana mna wajibu mkubwa wa kuisadia serikali kuwafichua mafisadi wote wa nchi hii ambao wanakwamisha maendeleo ya nchi, msaidieni Rais Kikwete ambaye hivi sasa ameamua kuwashughulikia mafisadi kweli kweli... vijana wa CCM fichueni ufisadi,"alisema.
Mkutano huo mkuu wa uchaguzi ulihudhuriwa pia na mgombea uenyekiti wa UV-CCM Taifa, Hamad Yusuf Masauni kutoka Tanzania Visiwani ambaye alifika kujitambulisha kwa wajumbe wa mkutano huo na vilevile kuomba kura.