kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Miaka 50 ya muungano imepita huku watanzania wakihoji kwanini kuna serikali ya Zanzibar lakini hakuna serikali ya Tanganyika, majibu yaliyokuwa yakitolewa kujibu swali hili yanapingana na majibu yanayotolewa na upande wa Zanzibar yanayodai kuwa Zanzibar ni nchi kamili iliyokuwa huru na yenye mipaka yake kamili na katiba, bendera na wimbo wa taifa wake.
Majibu yaliyokuwa wakipewa watanganyika yalidai kwamba Tanganyika ni nchi kubwa kuliko Zanzibar hivyo muungano ungeimeza Zanzibar. Majibu ya namna hii yaliwakanganya watanzania hasa watanganyika kwa miaka 50 sasa maana hayawaingii akilini. Hivi ni nani anayewaoenea huruma wa Zanzibar kuwa watamezwa na Tanganyika kwenye muungano wakati mipaka ya Zanzibar kama nchi inajulikana tangu awali kama ilivyo kwa mipaka ya vijiji, kata, wilaya na mikoa nchini inavyofahamika pia? Sijawahi kusikia mkoa wa Dar es Salaam umeumeza mkoa wa Arusha, Lindi, Mwanza wala Morogoro kwa jambo lolote.
Madaraka ya mkuu wa mkoa wa Mbeya yanajulikana na yale ya mkuu wa mkoa wa Kigoma yanafahamika pia. Sababu ya Zanzibar kumezwa na Tanganyika haina mashiko hata kidogo. Watanzania wanahitaji kufahamu kwanini muungano uwe wa serikali mbili na sio moja wala tatu. Hatutaki kuumiza vichwa vyetu kwa miaka 50 mingine tena kwa swali kama hili. Tunaomba sababu halisi ya serikali mbili CCM waiweke hadharani ili watu wote tuzijue, maana taifa hili ni letu sote sio la CCM.
Inavyoonekana wazanzibari hawataki serikali moja ambayo ndiyo ingeleta uimara wa muungano. Ili kuleta ulinganifu wa kinachotokea Zanzibar ni kubadilisha utawala wa mikoa ya Tanzania bara ijiendeshe yenyewe kwa asilimia fulani chini ya mkuu wao wa mkoa wa kuchaguluwa na wanamkoa wenyewe kama vile mkuu wa Zanzibar yenye watu mil. 1 anavyochaguliwa na Wazanzibari wenyewe.
Kisha tutahiyari jina la kumuita huyo mkuu wa mkoa aliyechaguliwa na wananchi wenyewe kama aitwe mkuu wa mkoa, rais wa mkoa au gavana, mtemi, n.k wa mkoa husika. Kisha kila mkoa uwe na sheria, kodi na taratibu zake kama ilivyo kwa Zanzibar. Mwisho wa siku tunakuwa na Rais mmoja tu wa jamhuri ya Tanzania mwenye heshima ndani ya nchi na kimataifa.
Bunge la katibu msije mkapoteza fursa hii adimu mkaja na katiba itakayolalamikiwa tena kwa miaka 50. tangulizenu utaifa mbele. Serikali mbili ni kwamanufaa ya nani?