TANZIA CCM Wilaya ya Geita yapata pigo, diwani Malimi Saguda afariki dunia

TANZIA CCM Wilaya ya Geita yapata pigo, diwani Malimi Saguda afariki dunia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita kimepata pigo baada ya diwani wake wa Kata ya Nyaruyeye Halmashauri ya Geita, Malimi Saguda kufariki dunia.

Malimi ameshika nafasi ya udiwani kwa vipindi viwili mfululizo na amefikwa na mauti akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Bugando kwa ugonjwa wa nimonia tangu Novemba 23, 2024.

1733490186740.png

Ni miezi minne imepita tangu diwani mwingine wa baraza hilo, Peter Kulwa aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari apoteze maisha.

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halmashuri ya Geita, Charles Kazungu amesema kifo hicho kilitokea jana Desemba 5, 2024 wakati akipatiwa matibabu jijini Mwanza.
 
Back
Top Bottom