LGE2024 CCM Wilaya ya Hai Yazidi Kuvuna Wanachama wa CHADEMA

LGE2024 CCM Wilaya ya Hai Yazidi Kuvuna Wanachama wa CHADEMA

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2024-11-23 at 14.17.32.jpeg

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro kimeendelea kuvuna wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaojiunga na CCM.

Hayo yamefanyika wakati wa kampeni zinazoongozwa na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe, ambapo wanachama wengi wa CHADEMA wameonekana wakijiunga na CCM huku wakikabidhi kadi zao na kupewa kadi mpya za CCM.


"Watu wanaoona CCM ndiyo yenye nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo hawana budi kuunga juhudi kwa lengo la kuijenga pamoja Hai yetu na Tanzania kwa ujumla" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

Mhe. Saashisha Mafuwe ameonekana na kusikika akinadi Sera za kistaarabu, akijikita kueleza kwa kina mambo mengi na makubwa yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kuwapelekea maendeleo wananchi wa Jimbo la Hai, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.

"Siasa safi ni ile inayoleta barabara, maji safi, miundombinu ya Elimu, huduma za afya, umeme na mambo mengine mengi muhimu ikiwemo kilimo" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai.

WhatsApp Image 2024-11-23 at 14.17.37.jpeg

Mhe. Saashisha Mafuwe amesema kuwa CCM haihitaji kujieleza sana, "ninyi ni mashahidi huko nyuma kabla hatujashika hatamu kwa jimbo hili, mliona tulivyokuwa wapweke, lakini oneni mambo tuliyofanya"

"Tuaminini tena katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa, tuweke mambo sawa kuwaletea maendeleo zaidi" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai
 
Back
Top Bottom