CCM ya Awamu ya Tano ilisamehe wengi akiwemo Kinana

CCM ya Awamu ya Tano ilisamehe wengi akiwemo Kinana

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
CCM mpya ya awamu ya tano haikuishia kuongoza kwenye kuwaletea maendeleo watanzania tu mbali iliongoza pia kwenye kutoa misamaha ya dhati kwa wanachama wake waliofanya makosa mbalimbali kwenye chama kipindi hicho.

Miongoni mwa misururu ya wanufaika wa misamaha hiyo ni pamoja na makamu mwenyekiti mpya bwana KINANA, wengine ni Nape, Makamba, Ngeleja, Sofia Simba etc.

Kwahiyo porojo zinazoenezwa na wanasiasa uchwara waliofilisika kichwani wa CHADEMA kwamba CCM ya Dk Bashiru, Dk Magufuli na Polepole iliongoza kwa ukatili wa kufukuza watu siyo kweli na ushahidi upo hadharani



 
Wenzenu waliamua kwenda madhabahuni na kumlilia Mungu wao, nanyi enendeni hivyohivyo mkatubu Kwa Mungu wenu mtasamehewa.
 
Huyo mtu wako unayeangaika kumtetea tunajua tayari ameshakufa mwache ajitetee mwenyewe huko alipo.
Kila mtu anajua jinsi alivyokuwa akijiona yeye ni mungu mtu,alipenda sana kunyenyekewa.
 
Nakubaliana nawe lkn tukumbushane pia kuwa ni CCM ya awamu ya tano hiyohiyo ndiyo ilianzisha mtindo wa kudukua mawasiliano ya watu kinyume na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kisha kuyatumia kuwahukumu.Tuendelee kukumbushana tu kuwa ni CCM ya awamu ya tano iliasisi mtindo wa kuwaruhusu vijana kuitisha press conference na kuwakashifu na kuwatukana wazee wetu waliolitumikia taifa hili kwa heshima.Ninaendelea kukumbusha tena kuwa ni CCM ya awamu ya tano iliyoasisi biashara ya watumwa kwa kuwanunua viongozi wa upinzani kwa bei ya kutupwa wakiwaacha watanzania katika dimbwi la umasikini.
Wakati Makonda anampiga ngumi Mzee Warioba awamu ya nne akapewa ukuu wa wilaya Kinondoni ulikuwa bado hujazaliwa?
 
Unayoiita CCM mpya ya Awamu ya 5 likikuwa ni genge la MWEHU mmoja toka Chato na ndugu zake akina Bashiru.

Mambo ya kishetani alivyofanya Magufuli asingeweza ku survive. Huwezi kuwatenga watu waliokupigania day and night ukawa Rais halafu unakuja kujaza washamba wenzio akina Polepole, Mpogoro, Bashiru, na Makonda!! Lazima UFE kifo chochote
Watu tunatafuta uwezekano wa kwenda kunya kwenye kaburi la Mwendazake pale Chato, wewe unaleta mambo yasiyomithilika.

Nimeamini ule msemo kuwa "hata wapumbavu huzeeka". johnthebaptist unazeeka kipumbavu
 
Kuna sisi chawa wa ngazi za chini hatufungamani na awamu yoyote...sasa hivi tunasimama na Kinana🐒🤸🤣
 
Wamerudi walikotoka
FB_IMG_16489763096268295.jpeg
FB_IMG_16489812603183801.jpeg
FB_IMG_16489762869580300.jpeg
 
Ni ajabu sana watu waliouza na kujibinafisha mali za chama leo hii ndio wamerudi kushika chama, na leo hii tunawasikia akina Makamba wakijinasibu kuwa katika awamu hii wanalamba asali, hiki chama ni kama genge fulani la kakikundi fulani ka walewa madaraka, inabidi sasa tuwaachie hii SACCOS yao. Tunawahitaji watu shupavu kutoka kwenye CCM kuikomboa tena CCM yetu ya mfanyakazi na mkulima na si ya hawa washihiri.
Shinda vijana wahumo wamenyeakambi,wasemavyo waswahili🤔.Kama kazi yao nikuimba pambio za sifa TU ili waonekane na kuongelewa mlo wao kwanini wasirudi wazee wenye hekima🧓
 
Sad to see this drop of moral behavior from the top guys. 100% wajiandae kusemwa na kudharaulika pia. Karma kama Karma
 
Back
Top Bottom