Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
Uandikishaji Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Wilaya ya Micheweni: Taarifa ya Awali Siku ya Pili 8 Julai, 2009
Watu 584 wanyimwa haki ya kuwa wapiga kura katika siku ya pili
Zoezi la uandikishaji wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Zanzibar lililoanza juzi katika wilaya ya Micheweni unaendelea katika hali ya mashaka. Ushirikiano ambao sisi katika Chama cha Wananchi (CUF) tunauita utatu usio mtakatifu (trinity of the demons) kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia masheha wake, Idara ya Vitambulisho na Tume ya Uchaguzi (ZEC) unaendeleza azma yake ya kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kuwa wapiga kura.
Katika rikodi zilizokusanywa juzi, wapiga kura 830 walinyimwa haki hiyo katika vituo sita vya jimbo la Konde huku wakiandikishwa 133 tu katika vituo vyote hivyo. Rikodi za jana zinaonesha kwamba watu 584 wamenyimwa haki hiyo na walioandikishwa ni 224 tu. Kwa hivyo, kwa juzi na jana tu, watu walionyimwa haki ya kuwa wapiga kura katika jimbo la Konde peke yake ni 1,414. Siku hizi mbili zilikuwa ni za uandikishaji wapiga kura wapya. Sababu inayotumika kwa ZEC kuwanyima watu hao haki ya kuwa wapiga kura ni kutokuwa kwao na vitambulisho vya Uzanzibari, sharti ambalo limewekwa na ZEC kwa kusudi maalum la kuvuruga uchaguzi.
Sharti hili liko kinyume na Katiba ya Zanzibar na misingi ya demokrasia ambayo nchi hii inajaribu kuijenga. Wengi wa watu walionyimwa haki hiyo wanazo shahada nyingine zinazothibitisha uzawa na ukweli kwamba wameshafikia umri wa kuwa wapiga kura.
Tunatuma taarifa hii ikiwa ni indhari ya namna hali inavyoendelea na makisio ya hali inakoelekea. Tutakuwa tukituma taarifa kila siku hadi kumalizika kwa zoezi.
Imesambazwa na:
Kurugenzi ya Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF