CCM ‘yachotewa’ na serikali Sh. 1.7 bilioni

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
MABILIONI ya shilingi ya umma yamechotwa kutoka hazina ya taifa kinyemela na kuelekezwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Hamisi Mguta.

Taarifa kutoka wizara ya fedha, Ikulu na ofisi kuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam zinasema, serikali imeitoa kiasi cha Sh. 1.7 bilioni kwa maelezo kuwa ni deni inalodaiwa na chama hicho tawala.

MABILIONI hayo ya fedha za umma yamechotwa kutoka hazina ya taifa kinyemela na kuelekezwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Hamisi Mguta.

Taarifa kutoka wizara ya fedha, Ikulu na ofisi kuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam zinasema, serikali imeitoa kiasi cha Sh. 1.7 bilioni kwa maelezo kuwa ni deni inalodawi na chama hicho tawala.

Kwa mujibu wa taarifa ndani ya serikali zinasema, chama hicho kimemiminiwa mabilioni hayo ya shilingi katika kipindi cha makusanyo ya mapato na matumizi ya mwezi Desemba mwaka huu.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameeleza katika waraka wake ambao MwanaHALISI Online umeuona kuwa serikali imelipa CCM fedha hizo, kwa kile ilichoita, “kufidia shule yake iliyotaifisha.”

Inayotajwa kuwa shule ya CCM ambayo imetaifishwa na hivyo kujaribu kuhalalisha malipo hayo, inafahamika kwa jina la “shule ya Sekondari Omumwani” iliyopo mjini Bukoba, mkoani Kagera.

Katika waraka wake huo, Dk. Mpango anaeleza, “kiasi cha Sh. 1,772,000,000 kinalipwa kwa ajili ya kulipia fidia kwa Jumuiya ya Wazazi wa CCM kutokana na Shule ya Sekondari Omumwani iliyopo Bukoba kutwaliwa na Serikali.”

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku mbili baada ya chama hicho kumaliza mkutano wake mkuu wa 19 mjini Dodoma.

Mbali na mkutano mkuu wa CCM, chama hicho kilifanya mikutano ya jumuiya zake tatu – wanawake, vijana na wazazi.

Kupitia mikutano hiyo, CCM inakadiriwa kutumia mabilioni ya shilingi bila kujulikana chanzo cha fedha hizo.
 
Awajaanza leo kuyafanya hayo mkohoji mtaitwa wachochezi
 
Ahsante kwa taarifa. Mimi na wewe hatuna hatia juu ya haya.
 
Nataman afisa usalama wa taifa mmoja mzalendo asimame na aseme ukwel kama yule wa USA
 
MABILIONI ya shilingi ya umma yamechotwa kutoka hazina ya taifa kinyemela na kuelekezwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Hamisi Mguta.

Taarifa kutoka wizara ya fedha, Ikulu na ofisi kuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam zinasema, serikali imeitoa kiasi cha Sh. 1.7 bilioni kwa maelezo kuwa ni deni inalodaiwa na chama hicho tawala.

MABILIONI hayo ya fedha za umma yamechotwa kutoka hazina ya taifa kinyemela na kuelekezwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Hamisi Mguta.

Taarifa kutoka wizara ya fedha, Ikulu na ofisi kuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam zinasema, serikali imeitoa kiasi cha Sh. 1.7 bilioni kwa maelezo kuwa ni deni inalodawi na chama hicho tawala.

Kwa mujibu wa taarifa ndani ya serikali zinasema, chama hicho kimemiminiwa mabilioni hayo ya shilingi katika kipindi cha makusanyo ya mapato na matumizi ya mwezi Desemba mwaka huu.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameeleza katika waraka wake ambao MwanaHALISI Online umeuona kuwa serikali imelipa CCM fedha hizo, kwa kile ilichoita, “kufidia shule yake iliyotaifisha.”

Inayotajwa kuwa shule ya CCM ambayo imetaifishwa na hivyo kujaribu kuhalalisha malipo hayo, inafahamika kwa jina la “shule ya Sekondari Omumwani” iliyopo mjini Bukoba, mkoani Kagera.

Katika waraka wake huo, Dk. Mpango anaeleza, “kiasi cha Sh. 1,772,000,000 kinalipwa kwa ajili ya kulipia fidia kwa Jumuiya ya Wazazi wa CCM kutokana na Shule ya Sekondari Omumwani iliyopo Bukoba kutwaliwa na Serikali.”

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku mbili baada ya chama hicho kumaliza mkutano wake mkuu wa 19 mjini Dodoma.

Mbali na mkutano mkuu wa CCM, chama hicho kilifanya mikutano ya jumuiya zake tatu – wanawake, vijana na wazazi.

Kupitia mikutano hiyo, CCM inakadiriwa kutumia mabilioni ya shilingi bila kujulikana chanzo cha fedha hizo.
Ndio maana m/kiti wazazi mzee bulembo alikuwa anatamba eti ameacha madaraka anakiachia bil 2. Kumbe kodi zetu? Hatari sana.

Kati ya watu walioharibu shule za wazazi, ni viongozi wa jumuiya hiyo waliomaliza muda wao. Nitashangaa kusikia wamerudishwa tena kwenye jumuiya
 
Watu waache kulipa kodi. Biashara zifungwe turudi vijijini tukalime ccm tuwaachie nchi. Hii inaumiza kusema kweli. So ndiyo pesa za kuhonga wabunge? Nchi imepata mchawi ambaye ni ccm.
Togo wapo na maandamano kila siku ni mwezi wa pili sasa wanasema mpaka kieleweke watu hawafanyi kazi.
 
Ndio maana m/kiti wazazi mzee bulembo alikuwa anatamba eti ameacha madaraka anakiachia bil 2. Kumbe kodi zetu? Hatari sana.

Kati ya watu walioharibu shule za wazazi, ni viongozi wa jumuiya hiyo waliomaliza muda wao. Nitashangaa kusikia wamerudishwa tena kwenye jumuiya

Mkuu ccm no janga LA Taifa
 
serikali imelipa CCM fedha hizo, kwa kile ilichoita, “kufidia shule yake iliyotaifisha.” Inayotajwa kuwa shule ya CCM ambayo imetaifishwa na hivyo kujaribu kuhalalisha malipo hayo, inafahamika kwa jina la “shule ya Sekondari Omumwani” iliyopo mjini Bukoba, mkoani Kagera.
..ambayo serkali iliikarabati (kwa kutumia fedha zilizochangwa wakati wa janga) la tetemeko la Bukoba mwaka 2016!
 
Back
Top Bottom