CCM yafuta matokeo ya uchaguzi wa UVCCM mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili wazi za rushwa

CCM yafuta matokeo ya uchaguzi wa UVCCM mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili wazi za rushwa

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Chama Cha Mapinduzi kimefuta matokeo ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili wazi za rushwa.

Dodoma. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefuta matokeo ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili za rushwa.

Mbali na Simiyu, lakini CCM kimesimamisha uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kwa mikoa ya Arusha na Mbeya ambao wanatuhumiwa kutembeza rushwa huku wakionya uamuzi wa kufuta unaweza kuendelea katika maeneo yatakayobainika kukiuka sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu Novemba 21,2022 na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Chongolo, leo ni siku ya tatu timu maalumu ya uchunguzi ipo huko ikichunguza zaidi kuhusu kilichojili ili vikao vifanye uamuzi.

Chongolo ametaja sababu kuu ni vitendo vya rushwa ambavyo vimetajwa katika maeneo hayo na kuwa chama hakitavulimia vitendo hivyo pale inapobainika.

"Mbali na hilo, tunachunguza kuhusu uchaguzi wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi katika tuhuma za kada mmoja kubeba boksi la kura kwenda nalo chumba cha kuhesabia kura ikibainika tutatoa maelekezo ama ya kufuta matokeo au kuruhusu aliyetangazwa aendelee," amesema Chongolo.

Kiongozi huyo ambaye ni mkurugenzi wa uchaguzi ndani ya chama amesema hawako tayari kuona viongozi wanaingia madarakani kwa rushwa na vitendo viovu.

Kuhusu adhabu zitakazotolewa alisema ni kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi na kupelekwa katika vyombo husika.

Chanzo: Mwananchi

Kwa hiyo yule mgombea wa uvccm aliyekuwa akigawa fedha kwa wajumbe, kwenye ile RAV 4 nyeusi yenye usajili wa C, ndiyo basi tena!
 
It's not fair kufuta uchaguzi kwasababu tuu clip ya rushwa imeonekana public kupitia mitandao ya kijamii.
Baadhi yetu humu ni wana CCM, CCM yetu ya kisasa tunaijua, na tunajua what it takes ili uchaguliwe, we all know the name of the game, and the games people play ili kushinda uchaguzi, hivyo tusifute chaguzi kwasababu tuu watu wamejua!
P
 
Shetani hana rafiki...ccm ya sasa ni rushwa rushwa tupu.

#MaendeleoHayanaChama
 
It's not fair kufuta uchaguzi kwasababu tuu clip ya rushwa imeonekana public kupitia mitandao ya kijamii.
Baadhi yetu humu ni wana CCM, CCM yetu ya kisasa tunaijua, na tunajua what it takes ili uchaguliwe, we all know the name of the game, and the games people plays kushinda, hivyo tusifute chaguzi kwasababu tuu watu wamejua!.
P
Kama kuna kitongoji, kijiji, Kata, wilaya au mkoa àmbao wagombea hawakutoa rushwa, NIKO TAYARI kuitwa Mbwa nimekaa paleee!
 
Kama kuna kitongoji, kijiji, Kata, wilaya au mkoa àmbao wagombea hawakutoa rushwa, NIKO TAYARI kuitwa Mbwa nimekaa paleee!
Hakuna rushwa CCM, kilichopo na kinachofanyikaga ni utoaji tuu wa fedha kidogo za uwezeshaji wa logistics support kama usafiri, nauli, kwa wana CCM waliopungukiwa nauli, na fedha kidogo za mchango wa kuimarisha chama, na kama una uwezo, hakuna ubaya wowote kuwakirimu wahumbe kwa kidogodogo cha takrima ya maji, soda, chakula na vitafunwa!. Hivi ndivyo siku zote tunavyo wa treat wajumbe wetu!

Wajumbe ni watu muhimu sana, lazima wawe treated ipasavyo.

P
 
Hakuna rushwa CCM, kilichopo ni utoaji wa uwezeshaji wa logistics support kama usafiri, nauli, na takrima ya maji, soda, chakula na vitafunwa.
P
Sasa anko Pasko, wewe kwenye lile "jambo letu" hakukua na logistics? Kwan wale jamaa walikua ngamia hawanywi maji?
Mbona kwako walikukwepa tukaishia kuona nyuzi ndeefu?

Usiwatetee bana. Call a spade a spade.
 
Huko Mkoa wa Kilimanjaro mgombea wa Nafasi ya mwenyekiti wa ccm mkoa na wajumbe wanaogombea nafasi ya Halmashauri kuu ya mkoa wamewagawia wajumbe fedha kama njugu
 
Hakuna rushwa CCM, kilichopo ni utoaji wa uwezeshaji wa logistics support kama usafiri, nauli, na takrima ya maji, soda, chakula na vitafunwa.
P
Kwahiyo kinachoendelea hapo Kwenye gari ni utaratiibu rasmi wa utoaji wa fedha za uwezeshaji wa logistics serious?

Hakuna chumba rasmi au utaratiibu rasmi wa kuwalipa watu wanaohusika na huo ulipaji na twapaswa kujua he ni fedha binafsi au zinatokana na mfuko au hazina ya chama kwamba zitatumika hivyo' na hivyo' ndivho zapaswa kutolewa kwa wahusika bila kutia saini Wala uthibitisho wowote wa malipo?

Je, mtoaji atafanyaje retirements kama huo ndio utaratiibu rasmi wa kuwezesha logistics support!

Na kama si Rushwa Chongolo anapata wapi uhalali wa kufuta hizo chaguzi?

Tabia hii wanakua nayo uvccm mpaka wanaingia jumuiya ya wazazi na UWT, kupitia chama kwa mtindo huo huo wanaomba ridhaa ya kuwa viongozi waandamizi na au kuteuliwa kushika nyadhifa muhimu serikalini.

Unadhani kwa tabia hii Rushwa na taarifa mbovu za CAG vitakoma? 10% Kwenye miradi itakoma?
Hii ni Cancer!

Adios!
 
Hakuna rushwa CCM, kilichopo ni utoaji wa uwezeshaji wa logistics support kama usafiri, nauli, na takrima ya maji, soda, chakula na vitafunwa.
P
Kwahiyo kinachoendelea hapo Kwenye gari ni utaratiibu rasmi wa utoaji wa fedha za uwezeshaji wa logistics serious?
Hakuna chumba rasmi au utaratiibu rasmi wa kuwalipa watu wanaohusika na huo ulipaji na twapaswa kujua he ni fedha binafsi au zinatokana na mfuko au hazina ya chama kwamba zitatumika hivyo' na hivyo' ndivho zapaswa kutolewa kwa wahusika bila kutia saini Wala uthibitisho wowote wa malipo?

Je, mtoaji atafanyaje retirements kama huo ndio utaratiibu rasmi wa kuwezesha logistics support !

Na kama si Rushwa Chongolo anapata wapi uhalali wa kufuta hizo chaguzi?

Tabia hii wanakua nayo uvccm mpaka wanaingia jumuiya ya wazazi na UWT, kupitia chama kwa mtindo huo huo wanaomba ridhaa ya kuwa viongozi waandamizi na au kuteuliwa kushika nyadhifa muhimu serikalini.

Unadhani kwa tabia hii Rushwa na taarifa mbovu za CAG vitakoma? 10% Kwenye miradi itakoma?
Hii ni Cancer!
Adios
hiyo ndio defence ya wakili, kama ccm inamawakili wa hivi bas ni tatizo.
Alitaka kugombea EALA akayaona haya akaona ni utaratiibu wa kawaida kama mwemdazake alivyohalalisha Rushwa ya Trafki! Kuwa ni kiwi
 
Hakuna rushwa CCM, kilichopo ni utoaji wa uwezeshaji wa logistics support kama usafiri, nauli, na takrima ya maji, soda, chakula na vitafunwa.
P
Kwa hiyo kilifanyika huko ni sawa tu siyo....
Kumbe ndomana wewe kila ukingia kutafuta nafasi unapigwa KO ,Inabidi sahv na wewe ufanye uwezeshaji huo

Ova
 
Tupige kura ya kukataa uwepo wa TAKUKURU, tuungane kuikataa ni hasara kwa taifa
 
Back
Top Bottom