Rugemeleza
JF-Expert Member
- Oct 26, 2009
- 668
- 136
Inaelekea mambo si mazuri hata kidogo huko Iringa mjini kwani hata gazeti la udaku wa kila siku Habari Leo linasema hivyo tafadhali jisomee!
Imeandikwa na Frank Leonard, Iringa;
Tarehe: 25th September 2010
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea na mikakati ya kilinusuru jimbo la Iringa Mjini lisiangukie mikononi mwa mgombea wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia anaonekana kuungwa mkono na baadhi ya wana CCM.
Hatua ya wana CCM hao kumuunga mkono mgombea huyo wa upinzani ni matokeo ya uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kumwengua aliyekuwa mshindi wa kura za maoni katika jimbo hilo, Frederick Mwakalebela na kumteua Monica Mbega, aliyekuwa mshindi wa pili kuwa mgombea.
Mbali na uongozi wa chama kuendelea kufanya vikao vya ndani kuwashawishi wana CCM hao kuvunja makundi ili kukipa ushindi wa kishindo chama hicho, siku mbili baada ya mgombea urais kupitia chama hicho, Jakaya Kikwete, kufanya kampeni zake mjini Iringa, alilazimika kurudi tena mjini hapa na kufanya kikao cha ndani na mabalozi na viongozi wa ngazi zote wa kata za jimbo hilo.
Lengo la kikao hicho kilichoelezwa kuanza saa tatu usiku badala ya saa 12 jioni kama ilivyokuwa imepangwa na ambacho wanahabari hawakuruhusiwa kuingia, lilikuwa ni kuvunja makundi yaliyotokana na kura za maoni na kuweka mikakati ya kukipatia ushindi.
Akitangaza kuvunja makundi katika mkutano wa kampeni uliofanywa Jumanne ya wiki iliyopita na mgombea urais wa CCM, aliyekuwa mshindi wa kura za maoni katika jimbo hilo, Mwakalebela alisema maendeleo makubwa yanayoonekana nchini kote ni matokeo ya utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM.
"Ndugu zanguni wapinzani wasitutumie kama mitaji yao ya kisiasa, natangaza kuvunja kambi na naomba wale wote waliokuwa wananiunga mkono sasa wakiunge mkono chama chetu kwa kuwapigia kura wagombea wote kuanzia rais, mbunge na madiwani," alisema huku akishangiliwa na mamia ya wananchi walioshiriki mkutano huo.
Wakati hayo yakijiri watu mbalimbali wakiwamo wana CCM na mgombea wa Chadema katika jimbo hilo, wameutilia shaka uamuzi wa CCM kumtumia Mwakalebela katika kampeni zake za ubunge mjini hapa.
"Haiingii akilini hata kidogo kwa sababu walipokuwa wakimwengua kuwania ubunge jimboni hapa, CCM walisema Mwakalebela hana maadili, amekifedhehesha chama na ni mtoa rushwa ambaye hawezi kusimama mbele ya wananchi kupeperusha bendera ya chama hicho na kwa sababu amefikishwa mahakamani kwa makosa ya rushwa, Mahakama iachwe ifanye kazi yake," alisema Mchungaji Msigwa.
Alisema mbali na kumfedhehesha Mwakalebela, CCM kama chama nayo inajifedhehesha kumtumia mtu ambaye tayari wanadai hana maadili na mtoa rushwa.
Naye mgombea udiwani wa Kwakilosa kupitia Chadema, Abou Changawa alisema zipo taarifa ambazo pia hazijathibitishwa, kwamba baadhi ya wana CCM wamemwomba Rais Kikwete kuingilia kati uhuru wa Mahakama kwa kuamuru kesi inayomkabili Mwakalebela ifutwe.
"Haya yote yanataka kufanywa ili kumsafishia njia Mwakalebela aingie katika kampeni zinazotokana na kudhulumiwa haki yake, naamini Kikwete ni mtu makini anayezingatia utawala na kwa wakati kama huu na mwingine wote, hatakuwa tayari kujiingiza katika mtego huo wa kuingilia uhuru wa Mahakama " alisema.
Chanzo Habari Leo: HabariLeo | CCM Iringa wahaha kunusuru jimbo