Elections 2010 CCM yakiri kupoteza viti 51

Kagalala

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
2,403
Reaction score
1,133
Kwa mujibu wa habari ndani ya Mwananchi, Bwana Kinana amekiri kuwa CCM imepoteza viti 29 Tanganyika na 22 Zanzibar.

Anasema urais wanashinda kwa asilimia 78.4. Hii inaonyesha jinsi gani matokeo yanavyopangwa na CCM jinsi watakavyo. Ametoa wapi hizo data kabla hayajatangazwa hata nusu ya majimbo?

Huu ni uhuni wa CCM.
 
Matokeo ya uchaguzi mkuu yanavyozidi kutangazwa imefahamika kuwa Chama tawala CCM kimepoteza m ajimbo 51 nchini kote.

Meneja wa kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana amekiri mbele ya waandishi wa habari mjiji Dar es Salaam leo kuwa CCM imemepoteza majimbo has 29 Tanzania Bara na majimbo 22 Visiwani Zanzibar.

Kinana amekiri kuwa athari ya kuanguka kwa CCM inatokana na migogoro ya kura za maoni .


Hata hivyo amesema CCM inatarajia kupata kura za rais kwa kiwango cha asilimia 78.4. Endelea kupata habari zaidi


Kutoka Mwananchi: 02 November 2010 02:23
 
Acha wewe kutudanganya. Mwaga ushahidi
 
Ukiri huo wa kinana una upungufu kidogo.peoples power ndiyo chanzo cha kushindwa popote kiliposhindwa chama cha mafisadiiii!
 
Jamani ingia mtandao wa Mwananchi utapata katiba breaking news zao
 

Hawa jamaa walichelewesha haya matokeo kwa kujitahidi kupanga na kuchakachua kura, naona wamekubali kuwa wayaachie majimbo hayo ndo maana anajidai kuongea... :A S angry:

Wameona mambo magumu wataaibika wakizidi kuchelewesha!!
 
Kinana amekiri kuwa athari ya kuanguka kwa CCM inatokana na migogoro ya kura za maoni .

Kwa kumsahihisha tu ni kwamba tatizo si tu migogoro ya kura za maoni vile vile ufisadi wao na umasikini wa wananchi
 
Kinana akiri ilikuwa vita kati ya wema na uovu, na kama kawaida waovu wameshindwa vibaya, grand finale 2015
 

Maji-taka
 
anataka kutuongopea huyu CHADEMA ndo wamepiga kazi sera zikakubarika kura ya maoni ndo nini
 
Mungu awaseme na kupofusha mawazo mabaya ya kuchakachua
 
Wana JF wote nisaidieni
Naombeni majina kamili ya wabunge wa upinzani (regardiless chama wa gani)
walioshinda ikiwezekana na majimbo yao, please help me
 
kaa mbali na sisi ustuambukize ujinga wewe ulietoa iyo mada
 
Matokeo ya uchaguzi mkuu yanavyozidi kutangazwa imefahamika kuwa Chama tawala CCM kimepoteza m ajimbo 51 nchini kote.Meneja wa kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana amekiri mbele ya waandishi wa habari mjiji Dar es Salaam leo kuwa CCM imemepoteza majimbo has 29 Tanzania Bara na majimbo 22 Visiwani Zanzibar.Kinana amekiri kuwa athari ya kuanguka kwa CCM inatokana na migogoro ya kura za maoni .

Hata hivyo amesema CCM inatarajia kupata kura za rais kwa kiwango cha asilimia 78.4. Endelea kupata habari zaidi.

Ni maneno ya kweli au ndio ushaanza uchakachuaji
 
Nadhani idadi ni juu zaidi ya hiyo ukijumlisha Bara na Visiwani
 
Huko bungeni watakoma hao ccm!
Kashfa zote zitaibuliwa...
 
Jamani someni hii attached file kuona mbinu na ufisadi uliofanywa na viongozi wetu kuhujumu uchaguzi. Halafu wanatuambia kwenye vyombo vya habari kwamba watu hawakujitokeza. Hii yote ilikuwa ni sabotage !! read the attached message

"Top secret from CCM!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…