Pre GE2025 CCM yakoshwa na uamuzi wa Mzee Baraka Shamte (BM) kwa kuweza kukwepa ghiliba na hadaa za upinzani

Pre GE2025 CCM yakoshwa na uamuzi wa Mzee Baraka Shamte (BM) kwa kuweza kukwepa ghiliba na hadaa za upinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Thabit Madai

Member
Joined
Oct 8, 2024
Posts
54
Reaction score
140
IMG-20241028-WA0091.jpg


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesifu ujasiri na uzalendo alionao Mwanassiasa Mkongwe Mzee Baraka Mohamed Shamte kwa kuweza kukwepa ghiliba na hadaa za upinzani na kuendelea kuunga mkono CCM.

Pia chama hicho kimesema uamuzi wake wa kuzungumzia maendeleo yaliopatikana kwa muda mfupi Zanzibar ameonyesha uungwana na kujua ukweli.

Msimamo huo umetolewa na katibu wa kamati Maalum ya NEC Idara ya itikadi na uenezi, Khamis Mbetto Khamis, aliyemtaja Mzee Shamte siku zote amekuwa mtu jasiri.

Mbetto alisema Mwasiasa huyo toka enzi za ASP baadae CCM,aliwahi kuteleza na kwenda kinyume na maadili ya chama akavuliwa uanachama wake.

'Amethamini juhudu za serikalivya awamu ya nane kwa hatua zinazochukuliwa na SMZ chini ya uongozi wa Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi. Taratibu za kumrudishia rasmi uanachama wake zitaelekezwa"Alifafanua Mbetto

Aidha allimtaja Mwanasiasa huyo ni mdau wa maendeleo hivuo kutokana na kuvutiwa kwake na ufanisi wa SMZ,ametokeza na kuonyesha hisia zake za kizalendo .

"Ameitumikia Zanzibar toka enzi za ukoloni .Amekuwa Naibu katibu mkuu ASP Youth League .Ameshakuwa katibu wa CCM wilaya. Mwenezi wa wilaya ya Mjini .Alipovuliwa uanachama hakubabaika .Amekuwa muungwana taratibu zitaelekezwa kumrudishia uanachama wake " Alisema Mbetto.

Aidha Katibu huyo Mwenezi alisema mzee huyo mara zote amekuwa akiitakia mema CCM,ndiyo maana hata alipofuatwa na baadhi ya vyama vya siasa wakimtaka ajiunge navyo , aliwakatalia .

"Ameona utendaji wa Seriiali ta Dk Mwinyi inavyochapakazi .Amekubali ukweli kutokana na dhamira yake ya kujenga nchi na kutumikia wananchi na nchi" Alieleza

Alisema CCM kwa kujua historia yake na mchango wake kwa Zanzibar ,hivyo maelekezo ya vikao vya kikatiba vitafanyika ili kutimiza matakwa na kutoa maazimio mengine.

"Awali hakutambua malengo na kusudio la Rais Dkt Mwinyi katika mtazamo wa muda mfupi na mrefu .Kujikwaa si kuanguka .Ameelewa ,amejisahihisha na sasa atashirikishwa kusukuma mbele jahazi la maendeleo "Alisema Mbetto.
 
Back
Top Bottom