CCM yamjulia hali muasisi wa TANU na mpigania Uhuru anayepatiwa matibabu MOI

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Jumapili 16 Januari 2022 Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amemtembelea na kumjuilia hali ya maendeleo ya afya yake Mzee Rehan B. Waikela aliyelazwa katika taasisi ya mifupa Muhimbili (Moi) akipatiwa matibabu.

"Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kinathamini na kujali kila mtu aliyejitoa na kujitolea kwa hali, mali, vitu, ujuzi na maarifa kufanikisha uhuru wa Nchi yetu na ukombozi wa Afrika. Mchango wao haupimiki wala hauwezi kuthaminishwa kwa chochote bali kwa kuwatambua, kuwajali na kuwatunza inaweza kuwa namna bora zaidi ya kutambua mchango wao.” Alisema Shaka.

Mzee Waikela amekuwa moja kati ya viongozi wa Chama cha TANU wakati huo ambaye alijitoa na kujitolea kwa hali na mali kuwapa ushirikiano wapigania Uhuru ili kufanikisha lengo hilo.

Historia inamtaja kuwa wakati viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, walipokuwa wakifika mkoani Tabora Mzee Waikela alikuwa akiwalaki kwa malazi, chakula na kuwapa huduma ya usafiri ili kuhamasisha harakati za Uhuru na Ujenzi wa Chama cha TANU wakati huo.

Pia soma > Bilal Rehani Waikela ni nani?

IMG-20220116-WA0058.jpg
IMG-20220116-WA0061.jpg
IMG-20220116-WA0060.jpg
 
Hapa chama kuchungulia faili la huyu mgonjwa aliye muasisi wa TANU/CCM wanataka kweli kumlipia bili ya matibabu au ni PR session? Chama kongwe kiwe wazi kuwaenzi waasisi wao kwa vitendo.
 
Huyo mzee ni miongoni mwa wale anao wazungumzia mara kwa mara Mohamed Said baada tu ya kupatikana uhuru walitupiliwa mbali na kuonekana si lolote si chochote lakini angalau mara hii wamempa heshima yake.
 
Huyo nae ana agenda zake za kidini!
Wazee walichangia kupatikana uhuru walikuwa ni wa nchi nzima, sio hao ndugu zake wa Kiriakoo tu, tena hao baadhi ya ndugu zake hawakufika hata Kibaha kuhamasisha wananchi kuhusu uhuru
 
Hapa chama kuchungulia faili la huyu mgonjwa aliye muasisi wa TANU/CCM wanataka kweli kumlipia bili ya matibabu au ni PR session? Chama kongwe kiwe wazi kuwaenzi waasisi wao kwa vitendo.

Kama Chama kinawapenda sana na kiwajali hao waasisi basi wawakatie Bima za matibabu za maisha, kuna na Yule Mzee Pia aliyemlizaga Nyerere kwenye mazishi yake
 
Huyo nae ana agenda zake za kidini!
Wazee walichangia kupatikana uhuru walikuwa ni wa nchi nzima, sio hao ndugu zake wa Kiriakoo tu, tena hao baadhi ya ndugu zake hawakufika hata Kibaha kuhamasisha wananchi kuhusu uhuru
Huyo sio wa kariakoo,huyo ni wa tabora alijitoa sana kwa hali na mali.
 
Jumapili 16 Januari 2022 Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amemtembelea na kumjuilia hali ya maendeleo ya afya yake Mzee Rehan B. Waikela aliyelazwa katika taasisi ya mifupa Muhimbili (Moi) akipatiwa matibabu.

"Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kinathamini na kujali kila mtu aliyejitoa na kujitolea kwa hali, mali, vitu, ujuzi na maarifa kufanikisha uhuru wa Nchi yetu na ukombozi wa Afrika. Mchango wao haupimiki wala hauwezi kuthaminishwa kwa chochote bali kwa kuwatambua, kuwajali na kuwatunza inaweza kuwa namna bora zaidi ya kutambua mchango wao.” Alisema Shaka.

Mzee Waikela amekuwa moja kati ya viongozi wa Chama cha TANU wakati huo ambaye alijitoa na kujitolea kwa hali na mali kuwapa ushirikiano wapigania Uhuru ili kufanikisha lengo hilo.

Historia inamtaja kuwa wakati viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, walipokuwa wakifika mkoani Tabora Mzee Waikela alikuwa akiwalaki kwa malazi, chakula na kuwapa huduma ya usafiri ili kuhamasisha harakati za Uhuru na Ujenzi wa Chama cha TANU wakati huo.

Pia soma > Bilal Rehani Waikela ni nani?

View attachment 2085164View attachment 2085165View attachment 2085167
Historia rasmi iliyoratibiwa ,kuandikwa na kufundishwa mashuleni haimtaji popote Mzee Waikela.Na hata hivyo baada ya uhuru alipata misukosuko mingi hadi kutiwa jela.Unamfunga Mbowe halafu kwa unafiki unajifanya kumjulia hali mtu mliyemtelekeza,kumfunga na kumfilisi.
 
Rais wa Tanzania anatakiwa ajiuzulu kwa kuhamasisha maofisa wa serikali kuiba pesa za umma.
 
Jumapili 16 Januari 2022 Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amemtembelea na kumjuilia hali ya maendeleo ya afya yake Mzee Rehan B. Waikela aliyelazwa katika taasisi ya mifupa Muhimbili (Moi) akipatiwa matibabu.

"Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kinathamini na kujali kila mtu aliyejitoa na kujitolea kwa hali, mali, vitu, ujuzi na maarifa kufanikisha uhuru wa Nchi yetu na ukombozi wa Afrika. Mchango wao haupimiki wala hauwezi kuthaminishwa kwa chochote bali kwa kuwatambua, kuwajali na kuwatunza inaweza kuwa namna bora zaidi ya kutambua mchango wao.” Alisema Shaka.

Mzee Waikela amekuwa moja kati ya viongozi wa Chama cha TANU wakati huo ambaye alijitoa na kujitolea kwa hali na mali kuwapa ushirikiano wapigania Uhuru ili kufanikisha lengo hilo.

Historia inamtaja kuwa wakati viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, walipokuwa wakifika mkoani Tabora Mzee Waikela alikuwa akiwalaki kwa malazi, chakula na kuwapa huduma ya usafiri ili kuhamasisha harakati za Uhuru na Ujenzi wa Chama cha TANU wakati huo.

Pia soma > Bilal Rehani Waikela ni nani?

View attachment 2085164View attachment 2085165View attachment 2085167
Huu ni unafiki kwa nini hawakwenda tangu mwanzo hadi shekhe ponda alipolalamika huko twiter ndo shaka kwa mashaka yake anajifanya kwenda.
Huyo mgonjwa amshukuru sana shekhe ponda bila hivyo hata asingejulikana.
Ugua pole mzee wetu.
 
Back
Top Bottom