Pre GE2025 CCM yampongeza DED Hai kwa kusimamia miradi ya maendeleo

Pre GE2025 CCM yampongeza DED Hai kwa kusimamia miradi ya maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Katibu wake, Ndugu Mercy Mollel amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Dkt. Haji Mnasi kwa kusimamia miradi ya maendeleo huku akiwaeleza wajumbe kazi kubwa aliyofanya DED Mnasi wakati akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ileje.

"Mkurugenzi yuko hapa huyu (Dkt. Mnasi) huyu nimefanya nae kazi mkoa wa Songwe alikua Wilaya ya Ileje alisimimamia ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya hadi baadae walitaka kuifanya ya rufaa. Msimuone mdogomdogo ana mambo huyu anafanya kazi nzuri." Alisema Katibu wa CCM mkoa akimpongeza DED Mnasi.

Pia soma: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Katibu Mercy ameyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa ilivyotembelea shughuli na miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Siha ambapo pia alipongeza utekelezaji wa haraka wa miradi katika Halmashauri hiyo.

 
CCM yampongeza DED Same kwa kusimamia miradi ya maendeleo
 

Attachments

  • millardayo_87586b7fde804f1793b45dcc73d99f50.jpg
    millardayo_87586b7fde804f1793b45dcc73d99f50.jpg
    180.4 KB · Views: 2
  • millardayo_a60d2b2aa8534d76a0ad5fc7153ab0cd.jpg
    millardayo_a60d2b2aa8534d76a0ad5fc7153ab0cd.jpg
    148.8 KB · Views: 2
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro,Boisafi mbona hayupo hapo????

Ila kifo ni kifo TU!
 
Back
Top Bottom