Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro kupitia Katibu wake, Ndugu Mercy Mollel amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Dkt. Haji Mnasi kwa kusimamia miradi ya maendeleo huku akiwaeleza wajumbe kazi kubwa aliyofanya DED Mnasi wakati akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ileje.
"Mkurugenzi yuko hapa huyu (Dkt. Mnasi) huyu nimefanya nae kazi mkoa wa Songwe alikua Wilaya ya Ileje alisimimamia ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya hadi baadae walitaka kuifanya ya rufaa. Msimuone mdogomdogo ana mambo huyu anafanya kazi nzuri." Alisema Katibu wa CCM mkoa akimpongeza DED Mnasi.
Katibu Mercy ameyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa ilivyotembelea shughuli na miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Siha ambapo pia alipongeza utekelezaji wa haraka wa miradi katika Halmashauri hiyo.