GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Wanabodi, Itikadi ni sera na uamini wa kile unachokisimamia bila kuyumba, CCM inaamini katika kujitegemea na ujamaa,Ujamaa katika CCM sio ule ujamaa wa mamlaka kuhodhi au kutwaa nguvu na rasilimali za wananchi bali ni ujamaa wa umoja na ushirikiano
Kuelekea uchaguzi huu wa 2020 neno ujamaa limepoteza maana kutoka na hali halisi inayoendelea kisiasa na kiuchumi,Hakuna ujamaa kama hali za wananchi zina hasira na vinyongo moyoni
Yafuatayo CCM inabidi iyafanye mapema wakati wa uchaguzi huu
Suala la TRA au mamlaka ya mapato Tanzania hapo kati inasemekana wameziandikia Benki notisi au barua nyingi sana kuhitaji pesa za wateja wadaiwa zipelekwe TRA, Benki inasemekana zilikuwa zina zuia akaunti za wateja yaani wana Freeze pesa isitoke bali iingie tu yaani No debit but Credit YES. CCM yapasa kulielezea suala hili kwa njia chanya zaidi ili kuwapooza hawa wafanyabiashara ambao ni wengi sana na wana madhara kwa ndugu na jamaa zao. Mfanyabiashara mmoja huwaambia watu zaidi ya 10,000 habari za kuumizwa na kodi na zote hizo ni kura
Suala la riba za mikopo kwa wanafunzi toka asilimia 8 hadi 15 limewakera na kuudhi wazazi wengi sana, Wazazi leo hawahudumiwi vizuri na vijana wao kisa madeni yamekuwa makubwa sana. Hili linajadiliwa sana ,Linahitaji suluhisho aidha riba ipungue
Suala la maendeleo ya vitu na sio maendeleo ya watu hapa ndio utata unaanza na ugumu kujibu hii hoja unaibuka,ccm yapasa kutoa ahadi za maisha bora wakati ujayo na sio kuelezea yaliyopita, Makampuni ya ujenzi yameumia sana hivyo ukisema umejenga zahanati kwa kutumia JKT ni dhahiri pesa kwenye mzunguko imerudi kwa mtoaji, Hapa CCM ijikite kwenye habari za maisha ya watu majukwaani
Suala la wakulima na mishahara kwa watumishi wa uma liongelewe kwa umakini mkubwa na kwa kuomba radhi kiujanja,Ni dhahiri mikoa ya wakulima wengi wanalalamika bei kushuka na wanashindwa kuuza mazao nje ya nchi kwani wamebanwa na wakubwa,Watumishi wa uma wanashangilia kinafiki tu hali zao sio nzuri sana,Yapasa kuwapunguzia riba ya Pay as you earn kwa kiwango kikubwa ili kufidia ya nyuma.