CCM yapeleka balaa mikutano ya Katiba

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
"CCM yapeleka balaa mikutano yaKatiba ; Waraka wake wazua tafrani Iringa"
Waraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanachama wake kushinikiza watetea matakwa ya chama hicho kwenye maoni yao katika mchakato wa Katiba Mpya umezua balaa, baada ya Mjumbe waTume ya Katiba kumzuia mmoja wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya kutumia waraka huo kutoa maoni yake. Alhaj Siad Elmamri ambaye kitaalamu ni mwanasheria, alimzuiaHussein Kiswil aliyekuwa akichangia mapendekezo kwenye rasimu hiyo, baada ya kubaini kuwa,alichokuwa anazungumza kilitokana na maelekezo ya CCM. Hata hivyo hatua hiyo ilizua tafrani katika mkutano huo, baada ya mjumbe huyo wa baraza la Katiba wilaya, kutoridhika na msimamo huo wa mjumbe wa tume na kupendekeza afukuzwe kwenye mchakato huo, kwa kile alichoeleza kuwa anapingana na maelekezo ya kuwaacha watu watoe maoni yao kwa uhuru. Kiswil alidai kuwa mjumbe huyo hastahili kuendelea na kazi ya kusimamia mabaraza hayo kwa kuwa yeye pamoja na wajumbe wenzake kadhaa, hawana imani naye. “Siku ya jana (juzi) tukiwa ndani ya ukumbi huu mlitueleza kuwa kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake katika kuchangia Rasimu ya Katiba hii, mimi nilichaguliwa kuingia katika kundi na kupewa jukumu la kuchambua muundo Muungano” alisema Kiswil na kuongeza; “Nilipoanza kuchangia mimi aliingiaMjumbe wa tume Elmamri na kusikiliza, nilipomaliza kabla hata ya kuruhusiwa na mwenyekiti alianza kuzungumza akisema maoni niliyotoa mimi ni maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi na aliongeza kuwa ana taarifa za kuwapo kwa kiongozi mkubwa wa kisiasa aliyekuja Iringa kutoa semina… nilitaka anithibitishie kama hayo aliyoyasema ni ya kweli.” Alisema kufuatia hatua hiyo ya mjumbe kushindwa kuthibitisha juu ya kuwapo kwa maelezo hayo kutoka CCM na suala la ujio wa kiongozi mkubwa wa CCM ngazi ya Taifa kuja kutoa semina alipendekeza kikao hicho cha Baraza la Katiba kujadili hoja hiyo aliyotoa na kutolea maamuzi. Akizungumza mara baada ya kupatiwa nafasi na mwenyekiti wa kikao hicho Omary Shahe Mussa, Elmamri alikiri kutoa ushauri kwa wajumbe kutumia nafasi hiyo kuchangia maoni yao badala ya maoni na msimamo wa chama. Alisema alitoa ushauri huo kufuatia kusoma kwake habari kutoka katika gazeti la Mwananchi iliyoelekeza maoni na msimamo wa Chama Cha Mapinduzi katika rasimu hiyo na kufafanua kuwa hata mjumbe alitoa yale yaliyokuwa yameshaandikwa na gazeti hili. “Mwenyekiti waTume Jaji Mstaafu Joseph Warioba alionya juu ya wanasisa kuacha wananchi kutoa maoni yao na alisisitiza kuwa vyama vya kuchangia maoni yao binafsi na si kutoka kwa viongozi wa vyama na kuongeza kuwa alifanya hivyo kutokana na msimamo uliokwishatolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Joseph Warioba. Wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti habari za CCM kusambaza waraka kwa wanachama wake ambao ni Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ngazi ya wilaya, kutaka wakisaidie chama hicho katika kutetea hoja zake kwenye mchakato wa Katiba Mpya. Pamoja na mambo mengine, chama hicho kimetofautiana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu Muundo wa Muungano, baada ya kupendekeza Muungano wa Serikalimbili badala ya serikali tatu. Hata hivyo mara kadhaa Mwe.nyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amenukuliwa mara kadhaa akipingana na misimamo ya baadhi ya wanasiasa kutaka kuingiza hoja zao kwenye Katiba Mpya kwa kutoa miongozi maalumu kwa wanachama wao. Jaji Warioba anasema kitendo hicho kitawaondolea watu uhuru wa kutoa mawazo yao.

© 2013 MCL
===
Warioba amnanga aliyetoa maoni kwa waraka wa CCM



Mwenyekiti wa Tume ya Mabadilikoya Katiba Jaji Joseph Warioba amewakosoa wajumbe wa mabaraza ya Katiba wanaokuja kwenye mikutano na matamko amanyaraka za vyama, badala ya maoni ya wananchi waliowachagua
Jaji alitoa kauli hiyo hiyo nzito wakati akifungua mkutano wa baraza la katiba katika Halmashauriya Musoma vijijini muda mfupi baada ya kundi la tatu kuwasilisha maoni yake.
Kauli ya Jaji Wariona ilikuja mara baada ya mjumbe Tobias Maugo kuchangia maoni kwenye rasimu ya Katiba akitumia waraka unaodaiwa kusambazwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanachama wake kikiwataka washinikize kupitishwa kwa mapendekezo ya chama hicho
Mjumbe huyo alikuwa akiusoma waraka huo neno kwa neno kana kwamba ilikuwa maoni yake mwenyewe.
Mjumbe unasoma waraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao sisi Tume tayari tunao mikononi mwetu. Hatukuzuia kusoma tena lakini nilitaka tu kukwambia kuwa kama una maoni mengine, uyasema kwa kuwa waraka huo tunao tayari.
Waraka wa CCM kwa wanachama wake umeanza kuleta tafrani ambapo juzi mkoani Iringa Mjumbe wa Tume ya Katiba alimzuia mmoja wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya kutumia waraka huo kutoa maoni yake.
Alhaj Said El-Maamry ambaye kitaalamu ni mwanasheria, alimzuiaHussein Kiswil aliyekuwa akichangia mapendekezo kwenye rasimu hiyo, baada ya kubaini kuwa,alichokuwa anazungumza kilitokana na maelekezo ya CCM.
Hata hivyo hatua hiyo ilizua tafrani katika mkutano huo, baada ya mjumbe huyo wa Baraza la Katiba wilaya, kutoridhika na msimamo huo wa mjumbe wa tume na kupendekeza afukuzwe kwenye mchakato huo, kwa kile alichoeleza kuwa anapingana na maelekezo ya kuwaacha watu watoe maoni yao kwa uhuru.
Kiswil alidai kuwa mjumbe huyo hastahili kuendelea na kazi ya kusimamia mabaraza hayo kwa kuwa yeye pamoja na wajumbe wenzake kadhaa, hawana imani naye.
Siku ya jana (juzi) tukiwa ndani ya ukumbi huu mlitueleza kuwa kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake katika kuchangia rasimu ya katiba hii, mimi nilichaguliwa kuingia katika kundi na kupewa jukumu la kuchambua muundo Muungano alisema Kiswil na kuongeza;
Nilipoanza kuchangia mimi aliingiaMjumbe wa tume El-Maamry na kusikiliza, nilipomaliza kabla hata ya kuruhusiwa na mwenyekiti alianza kuzungumza akisema maoni niliyotoa mimi ni maelekezo ya chama cha Mapinduzi na aliongeza kuwa ana taarifa za kuwapo kwa kiongozi mkubwa wa kisiasa aliyekuja Iringa kutoa semina Nilitaka anithibitishie kama hayo aliyoyasema ni ya kweli.
Kitendo cha CCM kuusambaza waraka huo kwa wanachama wake kinaelezwa kuwa ni kinyume na kanuni na utaratibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inataka watu watoe maoni yao wenyewe.
Tayari baadhi ya wajumbe wa Mabaraza ya Katika ngazi ya wilaya waliopata waraka huo wameripotiwa kuanza kuutumia kujenga hoja katika mijadala inayoendelea maeneo mbalimbali nchini.

© 2013 MCL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…