LGE2024 CCM yasambaza viongozi na makada waandamizi nchi nzima kuzindua kampeni Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Hamduni

Senior Member
Joined
Apr 25, 2020
Posts
172
Reaction score
118
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewasambaza viongozi wake wakiwamo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) katika mikoa 26 ya Tanzania kushiriki uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa kesho Jumatano, Novemba 20, 2024.

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuzindua kampeni hizo Mkoa wa Mwanza akiongoza viongozi na makada wa CCM waliotumwa maeneo mbalimbali nchini kwa kazi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya katibu mkuu wa chama hicho, Dk Nchimbi ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza, atazindua kampeni hizo katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Furahisha, Nyamagana, jijini Mwanza.
IMG-20241119-WA0043.jpg
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Mongella, atazindua kampeni Mkoa wa Mbeya, huku Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohamed Said Mohamed Dimwa, akizindua kampeni Mkoa wa Katavi.

Kampeni hizo zitaanza kesho Jumatano hadi Novemba 26, 2024 na uchaguzi utakuwa Novemba 27, 2024.

Viongozi wengine wa CCM waliopangiwa kuzindua kampeni ni pamoja na:
  • Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Oganaizesheni, mkoani Geita.
  • Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, mkoani Dar es Salaam.
  • Ndugu Rabia Himid Abdalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, mkoani Kilimanjaro.
  • Mhe. Dkt. Isdory Phillip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Dodoma.
  • Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Kigoma.
  • Mhe. Hemed Abdulla Suleiman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, mkoani Tanga.
  • Mhe. Zuber Ali Maulidi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mkoani Singida.

Viongozi wengine ni pamoja na:
  • Komredi Mary Pius Chatanda, Mwenyekiti wa UWT Taifa, mkoani Arusha.
  • Ndugu Mizengo Kayanza Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu, mkoani Mtwara.
  • Ndugu Halima Mamuya, mkoani Njombe.
  • Ndugu Nasir Ally Juma, mkoani Tabora.
  • Ndugu Mohamed Aboud Mohamed, mkoani Iringa.
  • Komredi Mohamed Ali Mohamed Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, mkoani Morogoro.
  • Ndugu Fadhili Maganya, Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, mkoani Simiyu.
  • Dkt. Dotto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu, mkoani Mara.
  • Ndugu Hussen Bashe, mkoani Shinyanga.
  • Ndugu Livingstone Lusinde, mkoani Manyara.
  • Ndugu Ally Hapi, mkoani Kagera.
  • Ndugu Nape Nnauye, mkoani Rukwa.
  • Ndugu Zainab Shomari, mkoani Lindi.
  • Ndugu Salim Faraji Abri (Asasi), mkoani Ruvuma.
  • Ndugu Jokate Mwengelo, mkoani Pwani.

- Richard Kasesela Mjumbe wa NEC, mkoani Songwe.

Mkakati huu wa kuzindua kampeni kwa mtindo wa ushirikiano wa karibu kati ya viongozi wakuu na wanachama unaonesha jinsi CCM inavyothamini uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Pia, unadhihirisha dhamira ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani, ambavyo hadi sasa vimeshindwa kusimamisha wagombea wa kutosha kushindana kikamilifu.
 
Attachments

  • IMG-20241119-WA0045.jpg
    IMG-20241119-WA0045.jpg
    663.3 KB · Views: 3
  • IMG-20241119-WA0041.jpg
    IMG-20241119-WA0041.jpg
    148.6 KB · Views: 3

Kwa uchaguzi gani hao makada wanasambaa? Au wanadhani kila mtu anaamini hizo hadaa?
 
Back
Top Bottom