CCM yatangaza mchakato wa uundaji mabaraza ya kata.

CCM yatangaza mchakato wa uundaji mabaraza ya kata.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,266
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza mchakato wake wa uundaji mabaraza ya Katiba huku kikisisitiza msimamo wake ni kuwepo serikali mbili.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Nape Nnauye, amesema, chama hicho kimeshaunda mabaraza hayo kuanzia ngazi ya matawi hadi mkoa.

Alisema kuanzia Agosti 20 hadi 25 , vikao vya taifa vya chama hicho, vitapitia mapendekezo ya mabaraza hayo kabla ya kuyawasilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Kwa mujibu wa Nape, kuanzia Agosti 20 hadi 23 kutakuwa na vikao vya Sekretarieti na kuanzia 24 hadi 25 kutakuwa na vikao vya juu vya taifa kwa ajili ya kupitia mapendekezo kabla ya kuwasilisha kwenye tume.

Akizungumzia msimamo wa chama wa kupinga kipengele cha Rasimu ya Katiba kinachopendekeza kuwepo kwa Serikali tatu, alisema msimamo huo hautakinzana wala kusababisha mvutano au ugomvi na makundi yenye msimamo tofauti.

Alisema tangu chama hicho kilipoweka hadharani hoja yake ya kupinga kipengele hicho na kupendekeza kuwepo na Serikali mbili, kumekuwepo na dhana potofu zinazosambazwa kwamba chama hicho, kina mvutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, jambo ambalo alisisitiza kuwa si kweli.

“CCM inaamini kuwa haiwezekani kutengeneza Katiba itakayofurahisha watu wote wakati mmoja, hivyo ni vyema kuheshimiana na kuvumiliana katika mjadala wa kuboresha rasimu hii…, hatuna ugomvi na tume wala mtu yeyote jambo la msingi tushindane kwa hoja,” alisisitiza Nnauye.

Alisema haimaanishi kwamba chama hicho kinapuuza na kugombana wale wenye hoja tofauti kuhusu kipengele hicho.

“Nasema hivi kwa kuwa kumekuwa na hoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari ambazo zinawaaminisha wananchi kwamba, kitendo cha CCM kupinga kipengele hiki kimesababisha kuwepo na mvutano baina yake na Tume ya Mabadiliko ya Katiba,” alisema.

Alisema chama hicho hakimshinikizi mtu akubaliane na mawazo yake na kwamba CCM kama taasisi inayo uhuru wa kuchangia rasimu, lakini yenyewe ni sehemu ndogo tu ya watanzania na iko tayari kuheshimu mawazo yao.

Chanzo: Habarileo.
 
Jukumu la CCM ni kuongoza na kuonyesha njia pale panapoonekana kuna utata katika safari ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kama ilivyokabidhiwa jukumu hilo na wananchi kwa mamilioni nchini mwaka 2010.

Kuna wengine kazi zao niza kuvizia kama fisi iwapo mkono wa kisiasa wa CCM utadondoka.

CCM ilithubutu, ikatenda na sasa inasonga mbele.
 
Hayo mabaraza yameundwa kujadili muungano tu. kwa sababu kitumbua kinataka kupokonywa mdomoni. Warioba songa mbele na watanzania tunakuamini katiba ni ya watanzania wote na si chama kimoja. Tunataka tukukumbuke maishani mwetu kwa zawadi njema ya katiba nzuri utakayo tupa. Mungu akupe nguvu na ujasiri wa kufanya kila liliojema katika katiba tunayoitengeneza
 
Jukumu la CCM ni kuongoza na kuonyesha njia pale panapoonekana kuna utata katika safari ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kama ilivyokabidhiwa jukumu hilo na wananchi kwa mamilioni nchini mwaka 2010.

Kuna wengine kazi zao niza kuvizia kama fisi iwapo mkono wa kisiasa wa CCM utadondoka.

CCM ilithubutu, ikatenda na sasa inasonga mbele.
Tunaandika katiba ya nchi na si katiba ya CCM kama nyie mnaona raha kuona neno serikali mbili mko huru kuendelea kuliandika kwenye katiba yenu ya CCM.
 
Acha kila mtu afanye mchakato wake.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
"hatutafanya kazi kwa mashinikizo ya vyama vya siasa" By Jaji Warioba
 
Back
Top Bottom