CCM yatoa maelekezo sakata la mgomo wafanyabiashara Kariakoo, Katiba Mpya


Zote hizo ni buying time tu ,kiini cha tatizo wafanyabiashara waliweka wazi ,kodi nyingi sana hadi nyingine zinajirudia rudia(Double taxation) ,Futeni kodi ya store ,kodi itozwe mara moja tu kwa mzigo ukiingia ,mlolongo mrefu wa kupata leseni na matozo kibao!! Kodi zinakusanywa nyingi halafu kina mwigulu wanaenda kuzipiga(mfanyabiashara alitoa maoni hayo ,akashauri wathibiti wizi ili wasiwe wanaumizwa wao kwenye kodi).
 
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba,Mwenyekiti wa CCM Taifa Mh Samia Suluhu Hassani ,amemuagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kwamba mgogoro wa Kariakoo, unadhibitiwe na kujua kiini cha tatizo...tena ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kikao...CCM Oyeee!
 
CCM wanajiona kuwa wanavyopeana PhD basi na akili wanazo, Kumbe umewasoma vituko vyao
 
Kwahiyo wanajiagiza wenyewe au Kuna misukule Wana iagiza? Au kwenye hiyo kamati kuu mwigulu hayupo pumbafu zenu
 
Mkuu meshawahi hata kuwa Class Monitor?
 
Wanacheza sana na akili za wananchi hawa CCM
 
Nimeandika humu marakadhaa kwamba serikali hutumia muda mwingi na pesa nyiongi kujifungia kutangeneza sheria, miongozo na tozo bila kuwashirikisaha wadau, (wafanyabiashara), matokeo yake huwa hayana tija ndiyo hicho kilichotokea kariako na kwingineko hili swala litakuwa endelevu kwasabu jamii yetu ni mfu ambayo haiwezi kuhoji
 
Nina mashaka na uwezo wetu wa akili
 
Yaani hii sijui imekaaje!! Walewale wenye migogoro na wafanyabiashara/kazi ndiyo Hao Hao wa nakaa na kujiagiza watafute suluhisho!!!! WOTE CHEKENI KWA SAUTI KUBWA HADI NEMC WAWAFUNGIEEEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…