Ccm yatoa miezi 6 kwa waziri wa elimu kujiuzulu..!!

Ccm yatoa miezi 6 kwa waziri wa elimu kujiuzulu..!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
[h=2][/h]
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kujiuzulu kwa kushindwa kulipa madeni ya walimu nchini.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pia ametoa muda wa miezi sita kwa Waziri huyo na Naibu wake Philip Mulogo kutekeleza hilo agizo hilo vinginevyo chama kitawatumia wabunge wake kuwatimua kwa nguvu.

Kwa mujibu wa taarifa za madeni zilizokusanywa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), hadi sasa walimu wanadai malimbikizo yao ya Sh bilioni 49 ambayo hajalipwa na Serikali.

Kinana alikuwa akihutubia mikutano ya hadhara jana katika wilaya za Bariadi na Busega.

Alisema CCM haiko tayari kuona walimu wakinyanyaswa wakati wana madai ya msingi.

Hivi sasa imejengeka tabia kwa baadhi ya mawaziri na watendaji wa wizara ya kuwadharau walimu na hata kuwanyanyasa huku wengine wakishusha utu na heshima ya walimu kwa kuwatukana, alisema.

Kinana ambaye yupo katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa alisema kwa mawaziri kushindwa kutatua kero za walimu, imefika wakati wahusika waondoke wenyewe na wasipofanya hivyo chama kitawaagiza wabunge wake wawafukuze kwa nguvu.

“Ninatoa muda wa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wakiwamo watendaji kuhakikisha wanalipa madeni ya walimu haraka. Haiwezeni hii ni nchi ya watu wote wakiwamo walimu wadharauliwe na hata kunyanyaswa kwa maneno ya matusi

“Hili hapana CCM haiko tayari kuona walimu kila siku wakipigwa danadana kutokana na uzembe wa watu waliokabidhiwa dhamana za kuongoza sekta ya elimu katika nchi yetu,” alisema.

MTANZANIA ilimtafuta Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch ambaye alisema hadi sasa madeni ya walimu yamefikia Sh bilioni 49 ambayo ni malimbikizo ya mishahara na mapunjo.

“Kila mara tunawaambia kuwa ni vema Serikali itafute Sh bilioni 100 katika fungu la dharura ili iweze kulipa madeni ya walimu na iachane nao lakini hawasikii,” alisema Oluoch.


-Mtanzania
 
Miezi sita ni mingi ambapo tutakua tunasubiri uchaguzi mkuu ata muda wao wa kuwa madarakani utakua unakaribia kuisha.
 
hizo zote ni njia tu za kutaka kutulaghai ili turudishe imani yetu kwao,maana miezi sita ni mingi sana kwahiyo muda wao wa madaraka utakua unaendea mwishoni.....




Ni hayo tu...!!!
 
KInana ana ubavu gani kumfukuza kazi binamu ya Rais? Hii nchi haiendi hivyo hilo ni changa la macho tu!!
 
walimu rahisi kuwalaghai kazeni uzi kama madactari

Ccm inalaghai tu hapo
 
Hypocrites hypocrites hypocrites!!! Serikali ya chama kipi ipo madarakani?
Je ilani ya chama cha Kinana inaongoza serikali ipi?
Walimu wameanza kulalamika kuwa hawalipwi na kunyanyaswa leo?
Mulugo na Shukuru wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata ilani ya chama kipi?
They are all hypocrites!!! Shame on you mulugo,shame on you shukuru,shame on you Kinana and shame on that party of yours!!
 
Vichekesho... Yaani serikali CCM inajipa yenyewe miezi sita kuwa imeshalipa hayo madeni..!!! Kwani aliyeyalimbikiza ni nani..??? Hawakawii kusema CDM ndo imelimbikiza madeni
 
Back
Top Bottom