Kada Mzalendo
Senior Member
- Oct 9, 2024
- 142
- 97
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ametoa wito mzito kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi na wananchi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi waadilifu na wenye moyo wa kuwatumikia wananchi.
Ametaka wagombea wanaoteuliwa wawe watu wanaopenda amani na utumishi, huku akiwakemea wale wenye chuki na visasi.
“Nyinyi wanaCCM mnatakiwa kutuchagulia wagombea wazuri, wanaojua kuwa uongozi ni utumishi. Mtu asiyependa watu na aliyejaa chuki hafai kuwa kiongozi wa wananchi,” alisema Dk. Nchimbi.
Aidha, amewataka wananchi waendelee kuiamini CCM kama chombo kinacholenga kuwaletea maendeleo endelevu. "Endeleeni kukiamini Chama cha Mapinduzi ili tuzidi kushika dola na kuongoza kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania," alihimiza Dk. Nchimbi.