Uchaguzi 2020 CCM Zanzibar imekata pumzi. Iko tayari kukubali yaishe??

Uchaguzi 2020 CCM Zanzibar imekata pumzi. Iko tayari kukubali yaishe??

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Asalam aleykum JFs

Hivyo ndivyo tunaweza kusema kuwa pumzi sasa ndani ya ccm na serikali yake imekata. Iko tayari kukubali yaishe. Katika moja ya habari inayosambaa mitandaoni kupitia Tv online ya Dar Mpya inaonesha katibu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu akiongea na waandishi wa habari akitababaisha kuwa Uchaguzi wa October 2020 Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha atakayepata kura nyingi ndiye atatangazwa kuwa mshindi.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na msuguano kila baada ya Uchaguzi Mkuu tangu mwaka 1995 ambapo Hamad Seif Sharif amekuwa akidai kushinda na kupokonywa ushindi. Lakini swali la kujiuliza ni je nani mwenye mamlaka ya kutangaza Mshindi?? Ni tume ya ZEC au Rais Magufuli??

Je tutakuwa sahihi tukisema kiwewe kinachopuliza huko CCM kutokana na kuimarika kwa upinzani Tanganyika na Zanzibar ndio kinaleta msukumo huo kwa Rais Magufuli?? Na je ni katika kujaribu kukwepa ule usemi usemao mtaka vyote kwa pupa hukosa yote, na ndio maana bora aelekeze nguvu Bara japo yeye abaki??

Je hili laweza kutokana na msukumo wa mabeberu kutokana na Ziara ya nguvu iliyofanywa na Viongozi wakuu wa ACT wazalendo duniani wakilalamikia ukiukwaji wa haki za kiraia Zanzibar??

Asante kwa Rais Magufuli kama amedhamilia alichokisema. Kwani ana dhima ya kuongoza nchi yenye amani na utulivu na hivyo atakuwa amewatendea watanzania haki yao ya msingi.

Wacha wapiga kura waamue.

CCM Zanzibar na walamba miguu yao tafuteni kazi nyingine kibarua kinafika mwisho October 2020.

Screenshot_20200525-103946_Chrome.jpg
 
Sio huko hata huku Bara pia ccm imekalia kuti kavu kuwa Bana wapinzani ndio pona Yao
Ni kweli viashiria vyote vinaonesha hivyo. Kwani hata watetezi hakuna wamebaki vyombo vya dola. Vyombo vya dola kamwe haviwezi kuleta ushawishi kwa Raia.
 
Back
Top Bottom