CCM Zanzibar kusimamisha shughuli mapokezi ya Dkt. Mwinyi

CCM Zanzibar kusimamisha shughuli mapokezi ya Dkt. Mwinyi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar kimewataka wanachama na wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiket ya chama hicho Dkt Hussein Ali Mwinyi ambae atawasili kesho Januari 22, 2025 mchana katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar

Katibu wa NEC idara ya Itikidi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea utaratibu wa mapokezi ya Mgombea huyo.

Soma Pia: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Amesema Mgombea wa CCM nafasi ya Urais Dkt Mwinyi atapokelewa katika viwanja vya ndege Zanzibar na kisha kupitishwa barabara hadi kufika Afisi kuu za CCM Kiswandui na baadae kuongea na wananchi na wanachama katika mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika Mapinduzi Square

 
Back
Top Bottom