Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalumu kuridhia kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kuongoza nchi katika muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohamed Said Dimwa
wakati akifunga mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya Dimami kichama Zanzibar uliofanyika Ofisi za Wilaya hiyo Kiembesamaki.
Dk Dimwa amesema uamuzi wa kumuongezea muda wa kuongoza Dk Mwinyi unatokana na kuridhishwa na kasi yake ya kiutendaji katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa zaidi ya asilimia 100 ndani ya kipindi miaka mitatu na miezi kadhaa tangu aingie madarakani.
Katika maelezo yake, Dk Dimwa amesema CCM Zanzibar imeona Serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa kuwa ni wananchi wanahitaji maendeleo endelevu, hivyo Rais Mwinyi anafaa kuongezewa muda ili Zanzibar iwe nchi ya visiwa iliyoendelea kiuchumi katika ukanda wa Afrika mashariki.
"Wajumbe wa sektetarieti tumejadili na kutathimini kwa kina juu ya utendaji wa Rais Mwinyi, tukajiridhisha hakuna mbadala wake na anastahiki aongoze nchi kwa kipindi cha miaka saba ili apate muda mzuri wa kufanya Mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii,” amesema Dk Dimwa.
PIA SOMA
- Hashim Rungwe: Kama tatizo ni muda, Rais Samia aongezewe muda ili tupate Katiba Mpya ndio tufanye Uchaguzi
- Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka
- Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono
- Mzee Mwinyi: Rais Magufuli aongezewe muda wa miaka 5 zaidi kama shukrani
- Zile kelele za Rais Magufuli aongezewe muda mbona hazipingwi kwa Rais Samia?
- Uchaguzi 2020 - Dkt. Magufuli aongezewe muda wa kutawala
- Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala