Pre GE2025 CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
#kataa machawa
 
Mara tu alipotamka maneno hayo, sauti kutoka mbinguni ikatamka: β€œEwe mfalme Nebukadneza, sikiliza ujumbe huu juu yako! Ufalme umekutoka! 32Utafukuzwa mbali na wanaadamu! Utaishi pamoja na wanyama wa porini kondeni, na utakula majani kama ng'ombe! Utakaa katika hali hiyo kwa muda wa miaka saba, na mwishowe utatambua kwamba Mungu Mkuu ndiye mwenye uwezo juu ya falme za wanaadamu, na humpa ufalme mtu yeyote amtakaye

Daniel 4:31
 
Huyu Bibi ni Mzambia, alikuja Zanzibar miaka ya mwanzo 1980 aliolewa na David Castico pale Kwa-Ali-Natu. Jambo la ajabu mwaka 2020 aliingia katika kinyang'anyiro cha kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM. Siku hizi amepotea haonekani..
Naongezea; kati ya mwaka 1999 na 2000 mwanzoni alikuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na alikuwa akimpigia chapuo Komandoo Salimu Amri aongezewe kipindi cha tatu cha uongozi Zanzibar. Akawa anasema Tanzania Bara hawawezi kutupangia tunachotaka. Baada ya Uchaguzi Mkuu, yaani 2001 Serikali ikatoa tamko kuwa huyu Mama si Mtanzania! Ahahahahaha!!!

Baadae aliombaomba msamaha, sasa hivi ni Katibu Mkuu wa CCM mkoa mojawapo hapa Bara! Sasa na huyu Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar awe makini. Historia hujurudia! Ahahahahaha!!!
 
Ata uku Bara kufanya uchaguzi ni kupotezea pesa,Mama ajiuzulu ili Mpango aapishwe until further notice!!
 
Wajumbe wa Sekretarieti ya kamati maalum ya chama cha Mapinduzi Zanzibar wamependekeza kuongezeka Kwa kipindi cha utawala kwa Kwa Rais Hussein Mwinyi kutoka miaka mitano mpaka saba.
Je Kuna ubaya au inafaa?
Ewe mjenga nchi tiririsha maoni yako
 

Attachments

  • FB_IMG_1719143807363.jpg
    39.2 KB · Views: 1
Wana mashaka ukifanyika uchaguzi 2025 kama atapita. Na atakayepita, kama Rais wa Muungano atakuwa Samia, hawana uhakika kama Rais Samia atakuwa radhi kuendelea kupora hela ya bara na kuinufaisha Zanzibar wakati Kaka yake akiwa ameondolewa kwenye Urais. Lakini wana uhakika kama Mwinyi akiendelea kuwa Rais Zanzibar, na kwenye Muungano akabakia Samia, lazima utaratibu wa sasa wa kuitumia Tanganyika kuijenga Zanzibar, utaendelea.
 
Sio kwa bahati mbaya!
 
Aahhh mbona Anachanganya Kati ya Masuala ya CCM na KATIBA .

Yaan CCM ZANZIBAR inataka uchaguzi wa kuchagua Rais wa Zanzibar anayeongoza Wananchi wa CUF, ACT, CHADEMA n.k... usifanyike????.


Bora Kwa JPM wetu hayo yalisemwa na Wananchi sio CCM.
 
Kwa kupitia katiba ipi!? πŸ™Œ Wana haki ya kuzungumza hivyo kwa kuwa midomo ni mali yao.
 
Kwa wakati huu hii ndo njia pekee watu wa kijani wanatumia kubakia madarakani kituo kinacho fuata ni kamati kuu ya Dodoma ila kwa hku sidhani kama watatoboa
 
Sithole country hapa mafisiemu yame ona yapime upepo kwa wapemaba kwanza ...useless state
 
Mungu wangu!. Ni utani au wako serious??! Mbona kama ni strategy ya kutumika nchi nzima! Kuanza na Zanzibar ni kisingizio tu. I hope wenye mapenzi mema na nchi bado wapo na hili halitafanikiwa.
 
Huu ulikuwa ni mpango wa dhalimu magu kabla Mungu hajaingilia kati, lakini mbegu matamanio yake imebaki hivyo inafanyiwa kazi.
Yani Mungu aingilie kati suala kama hilo tena kwa Tanzania tu? Hivi nyie huwa mnamchukuliaje huyo Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…