CCM Zanzibar jana Nov 2, 2024 walisherekea miaka 4 ya uongozi wa Rais Mwinyi pamoja na kuzindua kampeni ya Kijana na Kijani Pemba katika Uwanja wa Gombani, kampeni ambayo inalenga kuhamasisha vijana kupitia CCM kushiriki katika uchaguzi na nafasi mbalimbali za uongozi.
Kampeni hii ilizinduliwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa New Amani Complex Unguja Agosti 10, 2024.