CCM Zanzibar yataka chama cha ACT Wazalendo kuacha kuingilia kazi za Polisi

CCM Zanzibar yataka chama cha ACT Wazalendo kuacha kuingilia kazi za Polisi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka viongozi wa ACT Wazalendo kuacha pupa na papara ya kutoa maelezo yanayoingilia uhuru na majukumu ya vyombo vya dola, polisi na mamlaka zinazosimamia upelelezi

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo ,Khamisi Mbeto Khamis ambaye alisema CCM imesikitishwa kusikia maelezo yaliotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Zanzibar , Omar Ali Shehe , mara baada ya taarifa za vifo vya wananchi wawili huko Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba

Pia soma: Pemba: Polisi wachunguza vifo vya watu wawili waliofariki dunia wakipatiwa matibabu hospitali ya Ali Khamis Camp

Mbeto alisema matamshi ya kiongozi huyo wa ACT yanayomtaka Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi amfutekazi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala la Mikoa na Vikosi vya SMZ , kabla ya upelelezi kukamilika ni matamshi yaliokosa mantiki wala mashiko .

1735209725418.jpeg

Alisema kwa hekima na busara ni jambo jema kwa viongozi wa kisiasa kuviamini vyombo dhamana vinavyosimamia usalama wa ria na mali zao, kwani si kitendo cha kiungwana wanasiasa kuingilia kazi za upelelezi .

'Tunakiasa ACT Wazalendo na viongozi wake waache kufanya kazi zisizowahusu. Sisi viongozi wa yama tuna wajibu wa kuviamini vyombo vya dola . Kazi za kulinda na kusimamia amani na usalama wa raia ,hufanywa kwa uaminifu na polisi wetu si wanasiasa " Alisema Mbeto

'Viongozi wa kisiasa tuijue mipaka ya kazi zetu inapoishia. Ikiwa tunafanya siasa, basi kazi za upelelezi na uchunguzi wa kipolisi , tuwaachie polisi. Vinginevyo tubaki kwenye uwanja wa siasa , polisi nao wafanye kazi zao . Tusitake kupanda farasi wawili kwa wakati mmoja' Alieleza
 
Kwani huyo waziri ndiye anayefanya upelelezi,huyu jamaa anaongea mambo yasiyo husiana.
 
Back
Top Bottom