CDC: Dakika 150 za mazoezi mapesi zinafaa kwa wiki

CDC: Dakika 150 za mazoezi mapesi zinafaa kwa wiki

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Kwa mujibu wa Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa Cha Marekani (CDC), mtu mzima anashauriwa kushiriki mazoezi mepesi kwa walau dakika 150 kwa wiki.

Mazoezi huongeza utimamu wa afya ya mwili na akili, ni jambo jema katika kujikinga na maradhi ya mwili, hasa yale yasiyo ya kuambukiza.

Baadhi ya mazoezi haya ni kutembea kwa miguu, kuogelea, kuruka kamba, kutunza bustani pamoja na kuendesha baiskeli.

Faida zake-
  • Hupunguza hatari ya kuugua magonjwa ya moyo, kiharusi, kusukari pamoja na shinikizo kubwa la damu.
  • Huboresha mzunguko wa usingizi
  • Huongeza uwezo wa ubongo kwenye kutenda kazi zake hasa katika kufikiri na kutunza kumbukumbu
  • Husaidia kuweka sawa uzito wa mwili
  • Hupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya akili
Kutokujihusisha na aina yoyote ya mazoezi ni kikwazo kikubwa katika kutunza uthabiti wa afya kwa ujumla.

Kwa kuwa ni ngumu kushiriki mazoezi kila siku, dakika 150 zinaweza kugawanywa kwa siku 5 za wiki. Hii ni sawa na dakika 30 kwa siku.

Chanzo: CDC
 
Back
Top Bottom