CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

I like your analysis. Hii nchi haitawaliwi kijeshi. Inawezekana vipi makamu wa Rais ambaye ni second incharge kwenye utawala wa nchi awe ni mtu wa kupewa taarifa na CDF tena mbaya zaidi kwa kuchelewa? Familia ya marehemu iliachwaje hata pale marehemu alipozidiwa? Something fishy here.
 

Mkuu wa Majeshi huripoti kwa Amiri Jeshi Mkuu tu; hakuna cheo cha Makamu wa Amiri Jeshi Mkuu!
 
nimecheka kipuuzi sana!

ila Kitezo cha umeme kilivyo hakitoi udi ukakolea, itakuwa cha mkaa bana|!
 
Siamini chochote alichoongea jeneral!...kila alichoongea kimepangwa kwa sababu maalumu

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Hapa unamuonea bure CDF maana ktk utawala wa Jiwe hakukuwa na utawala wa Sheria

Alichofanya Jiwe ni kuwaweka watu wake karibu na kuwaongezea madaraka ya mdomoni ili wamlinde.
 
Cha msingi hapa ni kuwa Jiwe hayupo tena Tanzania
 
Wabongo kwa kupenda kukosoa hatujambo. Mzee wetu japo katupa mawili matatu kama namna ya kutufariji tayari ishakuwa nongwa! Acheni unafiki na ujuaji basi, mnafanya Viongozi wanakosa UHURU wa kutueleza mambo yenye msisimko kwa Viherehere vyenu.
Atufariji Kwa lipi mkuu?
 
Nakumbuka aliuliza eti mnafikiri Rais wa nchi anaweza kwenda sokoni kariakoo kununua mahitaji?
 
Mama anajuwa Kila kitu hakuna asichokijuwa kwenda tanga NI kiini macho Kila kitu alijuwa kinachoendelea
 
Kumbe hili jamaa sometimes linashushaga nondo nzito na kutema madini.

Mufti kuku The Infinity
 
Nimeshangaa pia:
  • Dar es Salaam walikuwepo watatu: CDF, IGP & DGIS
  • Makamu wa Rais alikuwa Tanga, Waziri Mkuu alikuwa mkoani (Dodoma or elsewhere)
  • Lakini Waziri Mkuu aliitwa na alipata taarifa mapema, kabla ya Makamu wa Rais
Something is fishy here.
Taifa ni kubwa kuliko mtu binafsi. Siku za usoni ni bora tukafiria njinsi ya kutengeneza mifumo bora. Kinacho tu beba ni busara na uvumilivu wa wenye nchi wananchi na ndiyo maana mawimbi na dhoruba zikitupiga tuna simama. Katiba mpya ni muhimu kwangu, kwako, na mwingine!
 
Magufuli aliweza kuagiza Mapadri waende, lakini alishindwa kuagiza aitiwe Makamu wake, hata amuachie wosia juu ya Majukumu anayomuachia, naona bado kuna vumbi halijatuama, nasubiri story zaidi.
Inaonekana kama Magufuli ndiye aliyekuwa hataki Makamu wa Rais ajue ugonjwa wake ukoje, na pengine alichangia au kuasisi mpango mzima wa kutaka katiba ipindishwe ili Makamu wa Rais asiwe Rais.

Hilo litakuwa consistent na Rais anayemtuma Makamu wake aende ziara mikoani wakati Rais anaumwa, na Rais ambaye anamuita Paroko na Kardinali lakini hataki kumuita Makamu wake aje kuwa pamoja naye wakati anaumwa vibaya sana.

Magufuli ameendeleza show ya kibabe mpaka mwisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…