CDF mstaafu Mabeyo amelikoroga, Makamu wa Rais ndiye alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kila hatua kujua afya ya Rais

Unajua kusoma na kuandika,lkn kina mambo mengi sana huyajui yaliyokuwa yakiendelea kipindi cha utawala wa awamu ya tano.
 
Kwa Kweli walimdharau mno mama, Nimefurahi alivyowatia adabu. Mpaka sasa wanaishi na machungu sana.
Kwani yeye atakaa hapo milele? Ile nikupokezana tu unamkomoa tu wewe ipo siku hata wajukuu wanaitubia hiyo dhambi
 
Mngejiuliza hiyo Mzena Hospital ni ya taasisi gani na madaktari ni WA taasisi gani na kwanini madaktari hawakupiga Kwa Makamu au PM hali ilivyobadilika wakapiga Kwa CDF, DGS na IGP.

Amiri Jeshi yupo hoi na katika hatua za mwisho na anauguzwa Mzena Hospital alafu wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wasiwe wanajua kinachoendelea wakati mgonjwa yupo Mzena Hospital

Btw kabla ya msiba wa kitaifa kutangazwa huwa kuna mambo nyuma ya pazia yanaendelea ilikuwa pamoja na way forward ili anaetangaza anakuwa amepata ABC za nini na nini cha kufanya
 
Wewe unazungumzia Matokeo, hujui root causes. CDF amefanya kazi yake ya kutufahamisha nia ovu ya Sukuma gang dhidi ya Mama Samia. Wakajisahau kuwa kama Mungu ameruhusu kifo kitokee yeye ndio anayeruhusu nani awe Rais
Kufa ni Mpango wa Mungu lakini sio kila kifo anapanga Mungu, Kwa kifo cha Magu(RIP Brother) ilikuwa sio rahisi kutangazwa chanzo walichosema.
Iko hivi kampuni za implants kama pace makers na vitu kama valves huwa ni guaranteed not to fail mpaka imalize masaa yake, sasa ikitokea imefeli hospitali waliofanya implant watajulisha vendor wao halafu wataona wao wanafanya nini.
Kutangaza kuwa pace maker ilifeli ni kuifilisisha kampuni husika, tungesikia kampuni fulani la vifaa tiba limeshuka thamani ya hisa zake au imefilisika, kwa sababu kwa namna yoyote wapinzani wao wange wa expose kuwa ndio mashine yao ilitumika tena kwa rais.
Nikupe mfano rahisi, wakati wa corona kulikuwa na ventilators , ikitokea umefia kwenye ile mashine kwa yenyewe kufeli kampuni itakulipa fidia kwa sababu zile ni aina za mashine ambazo zina deal na uhai wa mtu so policy yake iko hivyo.
Na hata ikitokea ventilator kufeli daktari hatakwambia labda uwe ulikuwepo ukawa mtu wa kuhoji na utake kuwashitaki ndio watakusilence kimya kimya maana ikijulikana tu hawana soko tena, hamna mtu atanunua mashine zao. Sasa hiyo ni ventilator tu vipi kwa Pace maker inayo deal na moyo?
 
Umenena vema mkuu, naungana na wewe.
 
Ifahamike pia kuwa, katika uhalisia, makamu wa Rais kwa Tanzania ni cheo kisichokuwa na uzito wowote. Ni mtu wa kutumwa. Asipotumwa, anashughulika na masuala tu ya Mwungano na mazingira
Hakika.
Makamu wa rais wa Tanzania ni sawa na 'mwanamfalme' anayesubiri kifo cha babake atwae madaraka.
Lakini ki uhalisia hana mamlaka makubwa.
Nalo limeacha funzo miongoni mwa viongozi.
Angalau sasa wanaipa heshima ofisi ya Makamu, maana tayari wameshajua rais anaweza kufa na yule wanayemdharau anaweza kukalia kiti cha uteuzi.
 
Kumbe Magu aliweza hadi kuwaita mapadri nyumbani baada ya kuona hali yake imedhoof? Na vipi kuhusu maneno ya kwamba alikauka kitambo tofauti na tarehe tuliyoambiwa na mama?
 
Inaonekana kuwa mpango mzima wa kumtenga Makamu wa Rais uliwekwa na Magufuli.

Tena ulianza kabla Magufuli hajaumwa.
 
Kwani hiyo ni hospitali ya nini? Kama hufahamu, ni heri ukakaa kimya. Serikali imeboresha sana hospital za jeshi.
 
Pia inaweza kua ni mbinu ya kiusalama. Maana kama watu hawakutaki, unajua wana kuwazia nn?
 
Kuna watu wanahisi Raisi na Makamu wake ni kama mke na mme, wako bega kwa bega
 
Makamo = Makamu. Ninadhani twende na alivyosimulia CDF na kama kuna mengine tunapaswa kujua basi ni suala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi.
 
Nimeshindwa kupata majibu sahihi kuhusu kifo cha JPM.

Kwanini ilishindikana kupelekwa London kutibiwa?

2. Mke wa marehemu na familiayake walijulishwa mumeweau baba anaumwa?

3. Katibu mkuu Kiongozi alikuwa wapi Rais akiwa anaumwa ?

4. Wakati Rais Yuko amelazwa, Makamu wa Rais aliibukia kwenye ziara mkoani Tanga, hii ziara ilipangwa na nani bila Rais kujua au bila makamu wa Rais kujua Rais Yuko Hoi kitandani:

5. Kwanini Katibu mkuu Kiongozi,aliengukiwa Ikulu siku 30 baada ya Kifo cha JPM?

Kifo cha mpendwa wetu JPM kina ulakini mkubwa sana.
 
Ameongea kipi kibaya? Unataka Mwamunyange aongeze kitu ambacho wakati kunatokea hakuwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…