CECAFA Challenge Cup

Ishaanza Kili 1 Burundi 1. Gozi linaendelea.
 
Vipi jamani mliopo bongo bado matokeo ni hayo hayo au kuna mabadiliko yoyote? Vipi uhai wa timu kiujumla?
 
Yani Burundi nao wanataka kutulambisha garasa...
 
Hii hatakua na heshima kabisa kwani wale jamaa wamekua kwenye kupigana muda mrefu, sasa sisi fani yetu ni nini? Au maneno? But hope will win this match
 
Duu, sasa tusishiriki mashindano ya soka manake tunatia aibu mno, Tukaendele na kazi yakuangua madafu pwani!!!!!!!!!
 
Inaelekea kuwa hivyo maana sasa ni Burundi 2-1 Kili Stars mpira ni mapumziko

Kazi bado ipo mbele yetu katika mashindano ya CHAN. Kama hali ndio hii tunayoona katika hili kombe, inabidi Maximo akaze buti, na hawa wachezaji wetu nao wakomae. Hawajui wako sokoni, tatizo wakipata sifa hujisahau. Nisilaumu sana mpira haujaisha, huenda tutashinda...
 
Si mpira wetu wa maneno ndo tumezoea.hapo hakuna mpinzani.
 
Maximo waambie vijana wakomae second half waTanzania tumechoka kuwa wasindikizaji kila mashindano, kwa mtindo huu kweli tutambulia chochote CHAN 2009 kule Ivory Coast?
 
Kwa mtindo huu tutakua wasindikizaji, labda madogo wa TSA watkapo anza vitu vyo nasi tutaonekana, maana niliwaona juzi wanaoenyesha watakua hai sana, kwani ni watakua maprofesional
 
According to Dullonet.com mpaka sasa Kilimanjaro 3 - Burundi 2. Huenda tukapata kifuta machozi.
 
Haahaaaa, weeee Kili lete rahaaaaaaaa, mbona itakua kama Barcelona juzi walisha lizwa 2 wakamchakaza mtu 3 mwishoni.
 
Ni kweli dakika ya 40 sasa tunaongoza 3-2 bao la pili la Kili stars limewekwa kimiani na Jerry Tegete, huyu ndio mshambuliaji wa kuaminika Kili na Taifa stars
 
mpira umeisha na tumeshinda.
Kilimanjaro 3 - Burundi 2

Sasa nguvu zetu kwa mashindano ya CHAN.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…