Uchaguzi 2020 Cecilia Mmbaga: Wauguzi wenye digrii hawataki kufanya kazi kijijini

Uchaguzi 2020 Cecilia Mmbaga: Wauguzi wenye digrii hawataki kufanya kazi kijijini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia Makini amesema wakiingia madarakani wataboresha huduma za afya ili kupunguza vifo vya wajawazito.

Amesema watawasomesha wasafishaji wa wodi za Hospitali ‘ward attendants’ kwa kozi za ukunga za miezi sita au miezi mitatu wakifuzu watapelekwa vijijini ili kuwahudumia wananchi wa huko.

Amesema wauguzi wenye digree na diploma wamekuwa ni watu wasiopenda kufanya kazi vijini hivyo wamekuwa wakitafuta sababu za kuhama kutoka huko.

Kutokana na hilo Demokrasia Makini inaona njia sahihi ni kuwasomesha ward attendants ili wakapunguze vifo vya wajawazito vijijini.
 
Hajui hata organogram ya wizara ya afya ikoje huyu.

Hajui hata levels of health facilities huyu!

Elimu ya mtu lazima iendane na facility husika.

Huwezi mpeleka specialist kituo cha afya wakati hakuna vitendea kazi vya level yake.

Yani ni sawa na kumpeleka brigedia akasimamie makuruta.
Unforgetable
 
Chadema wamezidiwa hoja na hiki chama.
Yaani akili ni ward attendant kwenda kuhudumia wajawazito na wanaojifungua?Si kuongeza vifo huko.
Ward/medicak attendant yake ni fagio
 
Yeye yupo kijijini? Kawawekea mazingira mazuri? Hao wa miezi 6 ili wakawamalize wajawazito na watoto au?
 
Daktari ni clinician, anaweza kufanya kazi hata huko vijijini, tatizo anazo pesa za kuwalipa endapo atawaajiri hadi ngazi ya kijiji na vipi kuhusu vifaa na dawa ambavyo vitawawezesha kufanya kazi huko na wasaidizi wengine kama manesi, technicians nk.
 
CHADEMA wamezidiwa hoja na hiki chama.
Chama kama DECI
Wanaishi kwa kujiuzakujiuza kwa wenye pesa, yoyote mwenye pesa anaweza kuwanunua ili aendeshe nchi, hawana dira wala maadili, wameachika kwa Lowasa sasa wamehamia kwa Amstadamz
Chama kimepoteza kabisa muelekeo tangu Dr Slaa agome kununuliwa
 
Back
Top Bottom