Cecilia Mwanga, Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia Makini amechukua fomu za uteuzi wa kugombea nafasi hiyo leo Agosti 8, 2020 katika ofisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma. Bi. Mwanga ameambatana na Mgombea Mwenza, Tabu Juma pamoja na viongozi wa chama.
Cecilia Mwanga, Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia Makini amechukua fomu za uteuzi wa kugombea nafasi hiyo leo Agosti 8, 2020 katika ofisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma. Bi. Mwanga ameambatana na Mgombea Mwenza, Tabu Juma pamoja na Viongozi wa chama.
Mgombea urais kwa tiketi ya Demokrasia Makini, Cecilia Augustino Mmanga aliyekwenda kuchukua fomu ya uteuzi wa kuwania urais NEC Makao Makuu wakiwa na Bajaji, Agost 8, amesema huo ndio utakuwa usafiri wao.
Amesema kwa kipindi chote cha kampeni kitakachoanza Agosti 26 wao watatumia Bajaji, pikipiki na baiskeli, guta na punda katika kufanya kampeni zao nchi nzima.
Akiongea na waandishi wa habari amesema watatumia usafiri huo kwa kuwa wakulima walio wengi ndio hutumia usafiri huo na wao chama chao ni Makini yaani makini ni maarifa, kilimo na nishati.