Cedric Kaze aonesha ubora wake mbele ya waajiri wake wa zamani Yanga

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Kwa namna mchezo ulivyopigwa leo hii kati ya Yanga na Namungo ni dhahiri kuwa Namungo waliwawin Yanga, na hii ni Ukomavu na ubora wa Kocha wa Namungo Cedric Kaze katika Usukaji wa Safu ya ulinzi.

Na kilichowafanya Yanga kushinda ilikuwa ni hali ya kupambana mpaka mwisho pasipo kukata tamaa.

 
Sema tu...Utopolo Wamepewa Goli La Offside, Yao alipokea mpira akiwa ameotea
Mbona tv imeonyesha alikuwa onside akawazidi mabeki speed na ujanja .
Namungo akicheza na yanga huwa anakamia tofauti na akicheza na wengine .
Katimu kanacheza rafu na vurugu nyingi kama wapo Kwenye ndondo yote kutaka sifa upande wa pili kuwa amemzuia yanga
 
Ulichoongea kina ukweli kwa 100%. Namungo walionesha upinzani mkubwa sana kwenye mechi ya jana. Hakika Yanga jana alipata mpinzani wa kweli.

Na wakiendelea kucheza kwa kiwango kila cha jana, basi nawategemea kwenye 5 bora. Hata goli walilofungwa, yalikuwa ni matokeo tu ya kucheza na timu kubwa.

Kwa upande wangu nilijua mechi ingeisha kwa sare ya 0-0.
 

Leo umeongea kimpira umeweka pembeni ushabiki.

Kongole [emoji1666][emoji1666]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…