Cement yao inanuka Shombo...!

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488
Mafundi ujenzi wa bongo kwa "swagga" hawajambo . Nilikutana nao site moja pale...wakiosha vifaa vyao vya kazi....mida ya jioni !
Mmoja alianza kwa kusema..." itabidi tuanze mgomo wa kutotumia sementi hii "...
Mwenzake akadakia kwa swali,.."Kwani vipi, Mbaba!?"
.."Sementi gani hii inanuka Shombo...,nimeosha vifaa nimeoga lakini bado ninanuka shombo kutokana na sementi hii" akajibu swali lile la fundi Mtwishe.
"Mwenzenu , shombo nilianza kulisikia toka boss alipotubadilisha siment juzi, nikadhani labda pua zangu zina wazimu..." Mtwishe huyo.

Saidia fundi, mmoja aliyekuwa anafuatili mjadala naye akadakia kwa kusema kuwa, alisikia siku moja watu wanasema sementi mpya, ingawa ni nafuu, ila inachanganywa na makaa ya mawe feki kutoka nje ya nchi na mtengezaji wa sementi hataki kuiosha na gesi asilia orijino inayopatika a hapa nchini kabla ya kuipakia kwenye viroba tayari kwa kuuzwa. Saidia fundi huyo aliongeza kuwa alisikia wanasema mtengenezaji anajaribu kupunguza gharama za uzalishaji....
ili apate faida kubwa

Mpaka hapo nilishindwa kuendelea kufuatilia maongezi yao.
 
utter cr@p
 
Naona kitengo cha propaganda ndo mmeamua kutoka na hii ya shombo ili kupotezea ishu ya kufungwa kiwanda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…