CEO wa Manaco atoa ya moyoni baada ya kumfuta kazi Thierry Henry

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
5,039
Reaction score
6,253
TAARIFA YA MONACO KUMFUTA KAZI THIERRY HENRY NA KUMRUDISHA LEONARDO JADIM

"Klabu yetu inapitia changamoto kubwa sana. Niko tayari kukiri kwamba mimi binafsi nawajibika kwa hali hii.

Tunapaswa kukiri wazi kwamba katika kipindi kikubwa cha usajili, tuliuza wachezaji wengi muhimu na, japo tuliwekeza vizuri kikosini, lakini kosa lililofanyika ni wachezaji sahihi wa kuziba nafasi za walioondoka.

Hili likatukwamisha kutengeneza timu mpya yenye ushindani. Uamuzi wa kumfukuza Leonardo Jardim ulikuwa wa kukurupuka.

Wakati wa Leonardo Jardim hapa AS Monaco, kama nilivyosema wakati tukimfukuza, utakumbukwa kama moja ya kurasa bora zaidi katika historia ya klabu.

Leo tumetambua kwamba hadithi ya Leonardo Jardim klabuni hapa ilikuwa haijakwisha kama ilivyopaswa. Leonardo alipaswa kupewa nafasi ya kuendelea na kazi yake.

Thierry Henry ni gwiji wa soka lakini kutokana na mjumuiko wa mazingira magumu ikwemo kuandamwa na majeraha kwa wachezaji wetu, akakwamishwa kuiongoza timu kwa haraka na mafanikio katika kipindi hiki kigumu.

Ningependa kutoa shukrani zangu za kipekee kwa Thierry Henry kwa kukubali changamoto hii na kujaribu kuiongoza timu yake ya zamani katika kipindi hiki kigumu.

Yawezekana alihitaji muda zaidi wa kutekeleza mipango yake. Kwa mtazamo wetu, ni bahati mbaya sana kwamba hatuna huo muda. Tunahitaji kuchukua hatua bila kuchelewa. Kwa hiyo, tumefanya maamuzi kufikia mwisho wa ushirikiano wetu na Thierry Henry.

Tulimfuata Leonardo Jardim na pendekezo la kurudi AS Monaco, ambako alifanikiwa kupata matokeo mazuri katika kipindi chake cha misimu minne. Tumeingia naye mkataba wa miaka miwili na nusu.

Makosa yaliyofanyika katika kipindi kikubwa cha usajili yamezingatiwa, na katika kipindi kidogo tumejitahidi kuimarisha kikosi. Tumejitahidi sana, na kama mnavyojua, wachezaji wapya tayari wameshajiunga nasi. Kipindi kidogo cha usajili hakijaisha na usajili mwingine mpya unaweza kufanyika.

Ni matumaini yetu kwamba hatujachelewa kulibaini tatizo. Ni imani yetu kwamba wachezaji wetu watashika kasi na kwamba, kwa pamoja na Leonardo Jardim kama kocha, ASM itaweza kukishinda kipindi hiki kigumu.

-Imetolewa na Vadim Vasilyev, makamu wa Rais na CEO, Monaco.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajji Manara jifunzeni sasa, yule kocha mnatimua mnaleta beberu matokeo mwayaona, rudisheni Omog na Masoud, pesa zenu zinatumika Hovyo kwa kuleta michezaji ambayo hata Mbao FC hawawezi ingia first eleven.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao wachezaji kina KULIBALI ambaye hata Alliance hawawezi kumsajili? Nadhani aliyemleta alikula 10% yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAARIFA YA MONACO KUMFUTA KAZI THIERRY HENRY NA KUMRUDISHA LEONARDO JADIM

"Klabu yetu inapitia changamoto kubwa sana. Niko tayari kukiri kwamba mimi binafsi nawajibika kwa hali hii.

Tunapaswa kukiri wazi kwamba katika kipindi kikubwa cha usajili, tuliuza wachezaji wengi muhimu na, japo tuliwekeza vizuri kikosini, lakini kosa lililofanyika ni wachezaji sahihi wa kuziba nafasi za walioondoka.

Hili likatukwamisha kutengeneza timu mpya yenye ushindani. Uamuzi wa kumfukuza Leonardo Jardim ulikuwa wa kukurupuka.

Wakati wa Leonardo Jardim hapa AS Monaco, kama nilivyosema wakati tukimfukuza, utakumbukwa kama moja ya kurasa bora zaidi katika historia ya klabu.

Leo tumetambua kwamba hadithi ya Leonardo Jardim klabuni hapa ilikuwa haijakwisha kama ilivyopaswa. Leonardo alipaswa kupewa nafasi ya kuendelea na kazi yake.

Thierry Henry ni gwiji wa soka lakini kutokana na mjumuiko wa mazingira magumu ikwemo kuandamwa na majeraha kwa wachezaji wetu, akakwamishwa kuiongoza timu kwa haraka na mafanikio katika kipindi hiki kigumu.

Ningependa kutoa shukrani zangu za kipekee kwa Thierry Henry kwa kukubali changamoto hii na kujaribu kuiongoza timu yake ya zamani katika kipindi hiki kigumu.

Yawezekana alihitaji muda zaidi wa kutekeleza mipango yake. Kwa mtazamo wetu, ni bahati mbaya sana kwamba hatuna huo muda. Tunahitaji kuchukua hatua bila kuchelewa. Kwa hiyo, tumefanya maamuzi kufikia mwisho wa ushirikiano wetu na Thierry Henry.

Tulimfuata Leonardo Jardim na pendekezo la kurudi AS Monaco, ambako alifanikiwa kupata matokeo mazuri katika kipindi chake cha misimu minne. Tumeingia naye mkataba wa miaka miwili na nusu.

Makosa yaliyofanyika katika kipindi kikubwa cha usajili yamezingatiwa, na katika kipindi kidogo tumejitahidi kuimarisha kikosi. Tumejitahidi sana, na kama mnavyojua, wachezaji wapya tayari wameshajiunga nasi. Kipindi kidogo cha usajili hakijaisha na usajili mwingine mpya unaweza kufanyika.

Ni matumaini yetu kwamba hatujachelewa kulibaini tatizo. Ni imani yetu kwamba wachezaji wetu watashika kasi na kwamba, kwa pamoja na Leonardo Jardim kama kocha, ASM itaweza kukishinda kipindi hiki kigumu.

-Imetolewa na Vadim Vasilyev, makamu wa Rais na CEO, Monaco.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kituko ni pale anayefukuzwa kazi ya ukocha anarudi kuwa football pundit na kuwasema makocha walio kazini.
 
Saev akienda pale sky sports atakua na soni kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha haaa nakumbuka kuna mechi 1 Gary Neville alikuwa anachambua. Timu moja ikapigwa 5-0
Gary Neville akasema,yeye angekuwa kocha kwa kipigo kile nyumbani angeshindwa hata namna ya kuongea na familia yake.
Mungu akajalia Neville akawa kocha wa Valencia,akaenda Nou Camp akala 7...
Hawa wachambuzi wakiwa makocha huwa wanashikishwa adabu sana.

Hahahhaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mendy, fabinho, benaldo Silva, bakayoko, mbape, Lemar, wameuzwa..

wakasajili nasir chadli, stefen jovetic, cecs fabregas!.. nadhani shida wamejua ilipo.. waache sera yao kuuza wachezaji bila kuwa na njia mbadala..
 
Back
Top Bottom