Alvajumaa
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 5,039
- 6,253
TAARIFA YA MONACO KUMFUTA KAZI THIERRY HENRY NA KUMRUDISHA LEONARDO JADIM
"Klabu yetu inapitia changamoto kubwa sana. Niko tayari kukiri kwamba mimi binafsi nawajibika kwa hali hii.
Tunapaswa kukiri wazi kwamba katika kipindi kikubwa cha usajili, tuliuza wachezaji wengi muhimu na, japo tuliwekeza vizuri kikosini, lakini kosa lililofanyika ni wachezaji sahihi wa kuziba nafasi za walioondoka.
Hili likatukwamisha kutengeneza timu mpya yenye ushindani. Uamuzi wa kumfukuza Leonardo Jardim ulikuwa wa kukurupuka.
Wakati wa Leonardo Jardim hapa AS Monaco, kama nilivyosema wakati tukimfukuza, utakumbukwa kama moja ya kurasa bora zaidi katika historia ya klabu.
Leo tumetambua kwamba hadithi ya Leonardo Jardim klabuni hapa ilikuwa haijakwisha kama ilivyopaswa. Leonardo alipaswa kupewa nafasi ya kuendelea na kazi yake.
Thierry Henry ni gwiji wa soka lakini kutokana na mjumuiko wa mazingira magumu ikwemo kuandamwa na majeraha kwa wachezaji wetu, akakwamishwa kuiongoza timu kwa haraka na mafanikio katika kipindi hiki kigumu.
Ningependa kutoa shukrani zangu za kipekee kwa Thierry Henry kwa kukubali changamoto hii na kujaribu kuiongoza timu yake ya zamani katika kipindi hiki kigumu.
Yawezekana alihitaji muda zaidi wa kutekeleza mipango yake. Kwa mtazamo wetu, ni bahati mbaya sana kwamba hatuna huo muda. Tunahitaji kuchukua hatua bila kuchelewa. Kwa hiyo, tumefanya maamuzi kufikia mwisho wa ushirikiano wetu na Thierry Henry.
Tulimfuata Leonardo Jardim na pendekezo la kurudi AS Monaco, ambako alifanikiwa kupata matokeo mazuri katika kipindi chake cha misimu minne. Tumeingia naye mkataba wa miaka miwili na nusu.
Makosa yaliyofanyika katika kipindi kikubwa cha usajili yamezingatiwa, na katika kipindi kidogo tumejitahidi kuimarisha kikosi. Tumejitahidi sana, na kama mnavyojua, wachezaji wapya tayari wameshajiunga nasi. Kipindi kidogo cha usajili hakijaisha na usajili mwingine mpya unaweza kufanyika.
Ni matumaini yetu kwamba hatujachelewa kulibaini tatizo. Ni imani yetu kwamba wachezaji wetu watashika kasi na kwamba, kwa pamoja na Leonardo Jardim kama kocha, ASM itaweza kukishinda kipindi hiki kigumu.
-Imetolewa na Vadim Vasilyev, makamu wa Rais na CEO, Monaco.
Sent using Jamii Forums mobile app