OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Baada ya Yanga kumtambulisha Andre Mtine kama Mtendaji Mkuu wao mpya nimepitia vyanzo mbalimbali vimeonesha kuwa ana rekodi za kesi na tuhuma mbalimbali.
1- KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA (2007) NDOLA, ZAMBIA ๐ฟ๐ฒ
- Andre Mtine alikamatwa na Mamlaka nchini Zambia kutokana na sakata la utakatishaji fedha wa kiasi na wizi wa kiasi cha Kwacha Million 100 sambamba na Maofisa wawili waandamizi ndani ya benki ya Posta ya Zambia.
Wahusika walikuwa Mtine, 43, a Football Association of Zambia (FAZ) Finance manager, Gilbert Kapambwe, 42 na Financial accountant Ignatius Kapembwa.
[Chanzo: The Times of Zambia ]
2- KUKAMATWA NA MAMLAKA ZA UHAMIAJI ZAMBIA ๐ฟ๐ฒ 2013
Mtine alikamatwa na Mamlaka za Uhamiaji nchini Zambia mnamo tarehe 18- 10- 2013 majira ya saa 6:30 mchana kutokana na kuvunja sheria za Uhamiaji kwa wachezaji watatu Stopilla Sunzu, Nathan Sinkala na Reinford Kalaba ambapo baadae waliitwa kutoa maelezo na wakaachiwa.
[Chanzo: Lusaka Voice]
3- KUKAMATWA NA MAMLAKA KUHUSU WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA ๐ฟ๐ฒ (2014)
- Mtine inasemekana alishawishi wachezaji Nathan Sinkala na Stopilla wasusie mechi ya timu ya taifa ya Zambia dhidi ya Japan, huku pia FAZ wakisema wazi yeye ndie chanzo cha mgogoro kati yao na klabu ya TP Mazembe.
Alifungiwa maisha kujihusisha na soka nchini Zambia.
[ Chanzo: Lusaka Voice]
My Take
Ina maana Utopolo hamkumgugo huyu mtakatisha fedha? Au mmemchukua kimkakati kama mtalaam mwenye uzoefu wa kupiga?