Certificate of general agriculture and certificate of animal health and production ipi ni nzur?

Certificate of general agriculture and certificate of animal health and production ipi ni nzur?

Asu tz

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2011
Posts
336
Reaction score
86
Habr wana jf natumain mpo vema na mnaendelea na harakat za maisha ya kila siku.

Samahan wakuu naomba kujuzwa ipi ni koz nzur kat ya hzo hapo juu nina mdogo wangu amepata chuo cha kilimo kaole bagamoyo.
Ameniomba ushaur nikaona niulete hapa jf kabla sijajua nitamshaur nn

Nawasilisha kwenu wakuu.
 
vyuo vingi vya private ni magumashi hata wakufunzi wa kutosha hawana, chuo cha Bagamoyo nafikiri ni private na ndio kinaanza, ila hilo nafikiri si tatizo sana fuatilia ujue kama kimesajiliwa na NACTE au VETA.Kama kimesajiliwa, wakufunzi wapo wa kutosha na wenye sifa stahili kwa upande wa hiyo kozi binafsi naona ni relevant ukilinganisha na AHPC kwani vijijini hawajui kama kuna mtaalamu wa mazao tu/mifugo tu wao wanachokielewa ni kwamba bwana/bibi shamba anaelewa kila kitu kinachohusiana na kilimo dhana ambayo ni sahihi sana.
 
chuo kimesajiliwa na nacte namba ya usajil n 86834 oct 2011.
Nashkuru kwa mawazo yako mkuu.
 
nyongeza..nadhani agriculture genral ni ishu..ila hiyo ya animal iko too specific..
 
Mwambie asome Agriculture general!Ipo wide sana ambapo pia ndani yake atasoma animal production na mengineyo!Yaani ni 2 in 1.
 
shukran wakuu kwa mawazo yenu.
 
vyuo vingi vya private ni magumashi hata wakufunzi wa kutosha hawana, chuo cha Bagamoyo nafikiri ni private na ndio kinaanza, ila hilo nafikiri si tatizo sana fuatilia ujue kama kimesajiliwa na NACTE au VETA.Kama kimesajiliwa, wakufunzi wapo wa kutosha na wenye sifa stahili kwa upande wa hiyo kozi binafsi naona ni relevant ukilinganisha na AHPC kwani vijijini hawajui kama kuna mtaalamu wa mazao tu/mifugo tu wao wanachokielewa ni kwamba bwana/bibi shamba anaelewa kila kitu kinachohusiana na kilimo dhana ambayo ni sahihi sana.

Mkuu, hapo kwenye blue and bold. Mtazamo huo sio sahihi kabisa. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kilimo na mifugo. Hata kwenye mifugo tu kuna tofauti ya aliyesoma uzalishaji (production) na Afya ya migugo/wanyama (Health). Watumishi wengi wa kilimo na mifugo wanatumia kutojua kwa watu vijijini kuwadanganya na kufanya madudu ya ajabu sana. Kwa bahati mbaya sana, kiutendaji wakulima wanahitaji sana huduma za afya ya mifugo. Pia kuna aina za uzalishaji ambazo zina soko kutegemeana na mahali mtu alipo. Hizi ni kama Uhamilishaji (Artificial insermination).

Afya ya mifugo ni taaluma kama udaktari wa binadamu na hawa watumishi wa chini ni kama Medical assistants, clinical Officers, nurses na Health officers. Kwa kutojua, watu waliosoma Kilimo wanatibu magonjwa ya wanyama ka kujichukulia pesa za wakulima. Hii si sawa kabisa kwani kwa kufanya hivyo, wanaathiri mbinu na mikakati ya kuondoa magonjwa ya wanyama na hata kuathiri afya za binadamu.

Huwezi ukasoma kilimo (vipando) ukatibu wanyama!!!! wala kukagua nyama. Nahisi ndio sababu mwaka 2007 wakati wa homa ya bonde la ufa watu wengi waliathirika (hata kufa) kwani wakaguzi wa nyama wengi ni vihiyo. Hawawezi kujua nyama iliyoathiriwa na ugonjwa wowote kwa kuwa hawakusomea.
 
Back
Top Bottom