it sound gud hapo kwenye red na muda wenyewe nahisi ndio unakaribia maana kwa mienendo ya ndoa zetu za sasa ni hatari tupu!C kama wafuasi wa CCM, walionzisha chama wanachukizwa nacho ila wafuasi waliokipokea huwaambii kitu! Ni uelewa mdogo, na kufundishwa kupokea tu bila ya kutafakari kwa kina! hawa makasisi wetu wanatupa dozi nyingi isoyomwezesha mpokeaji kufikiri kwa undani, ila nafikri ni swala na muda tu hata sisi waafrika tutafikia huko kwa wenzetu.
na yameisha kweli, ni wachache sana wanaopenda kwa dhati,mmmh my dia mm naona kama mapenzi yameisha yameisha tu,hata msipo andikishana au muandikishane mbele ya papa!
Mimi mara nyingi hujiuliza kabla kuja kwa Mzungu/Mwarabu, sisi waafrika hatukuwa na dini zetu??, Ni hizo dini zetu ziltuasi nini kwa mambo ya ndoa?, Kuuliza hivi ni kwa sababu..wakati wa mababu zetu, mwanaume alikuwa anao zaidi ya mke mmoja, kulingana na uwezo wake. Wako wengi nafikiri walikufa wakiwa na wake moja moja. Kaja mzungu , ooohh tuombe fungeni macho, tukifungua macho....mashamba yashakwenda. Mzungu na mwarabu alitufundisha DINI, lakini woote hawa hawafuati hizo dini wenyeweeee!!!!
Suluhisho ni kufuata dini......(Fuata uambiwayo, sio uonayoooo!!!!)
ninayajua yote hayo ila kwa mujibu wa taraibu zetu za dini esp ya kikristo, ukishafunga ndoa ndio basi, huwezi kufunga tena, hata mkitengana labda afe.Kama hakuna mapenzi, hata hiyo ndoa haitokuwapo... hizo nyingine ni taratibu tu!!!!
Kwa mujibu wa historia niliosoma o-level na shule ya msingi pia, dini ililetwa na ndugu zetu wazungu enzi hizo,
swali langu ni hivi, wao waliotulea dini ndoa zao hazina ugumu kwenye divorce hata kama ni za kanisani, sisi tuliopokea dini tunakomaa na "alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe" wakuu nisaidieni mawazo, hii mnaionaje?