chachas mchina: hivi ni lipi sahihi.

chachas mchina: hivi ni lipi sahihi.

Joined
Jan 2, 2012
Posts
33
Reaction score
0
Kuna gazeti moja hivi, wameandika kuwa mwakyembe atoa Wakala, sasa ni wakala au ni walaka?? nisaidieni hapo.
 
Kuna gazeti moja hivi, wameandika kuwa mwakyembe atoa Wakala, sasa ni wakala au ni walaka?? nisaidieni hapo.

Haya ni matatizo ya kila siku ya "r" na "l".
Neno husika lilitakiwa liwe "waraka" yaani ujumbe
Kwa hiyo sentenso yote ilipaswa isomeke 'Mwakyembe atoa waraka' Mjomba wangu anavilalamikia sana vyombo vya habari, hasa magazeti kwa sababu waandishi wake hawako makini na lugha ya Kiswahili.Jina la mjomba wangu kwa mfano ni Selestine Marya, lakini alipopeleka barua ya maoni kwenye gazeti moja, wakachapisha barua na kuandika jina la mwandishi: "Serestine Malya" - jina jingine tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom