SoC02 Chachu ya mabadiliko katika kilimo

SoC02 Chachu ya mabadiliko katika kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

Nyakibeku

New Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
1
Reaction score
0
CHACHU YA MABADILIKO KATIKA KILIMO
Na Amini Nyaungo

Kilimo ni shina la maisha ya Watanzania waliowengi hutegemea chakula chao kupitia kiimo. Kiwango kikubwa tunategemea kilimo.

Lakini bado kila mmoja anajiuliza kila siku tunategemea kilimo ambacho hakina tija na wakati mwingine kupata chakula ambacho hakifiki msimu unaokuja.

Unafikiria hii inaweza kuinua maisha ya Mtanzania bila ya kuwa na uwezo wa haraka wa kufikiria ili tuweze kuapata chakula lakini maendeleo katika maisha yetu ya kila siku.

Hapa nitaangalia sehemu tatu ambazo kama tukishirikiana kwa pamoja basi kila mmoja atapata maendeleo, sehemu hizo ni pamoja na Serikali, Wakulima na Wafanyabiashara. Hizi sehemu ni muhimu sana na utanielewa kile ninachotaka kukilenga ili tuweze kufika katika maendeleo ya kweli huku baa la njaa haliwezi kutufikia.

SERIKALI, hawa ndio kitovu cha kutengeneza wakulima ambao wataweza kuondokana na kilimo ambacho hivi sasa tunaendelea nacho na kuja katika kilimo chenye tija na maendeleo.

Serikali ifanye nini ili iwasaidie wakulima ? Awali kabisa Serikali inatakiwa itoe ruzuku ya mbegu kwa wakulima ili wafike sehemu ambayo itaweza kuwa msaada kwao , mbegu zenyewe ziwe za kisasa zinazoendana na hali ya hewa na sehemu husika.

Serikali inatakiwa iwatafute watafiti wa kilimo kwa kushirikiana na Maafisa kilimo kuwaongoza Wakulima wajue mbinu bora za kilimo.

Bila shaka tunapaswa kujua kilimo cha kiikolojia kilimo hiki kinaleta tija kwani hakitumii madawa bali kinalimwa kwa kutumia mbinu bora lakini pia hata mtumiaji atakayetumia bidhaa iliyolimwa na kilimo cha kiikolojia hatopata madhara kwani kilimo chake hakitotumia dawa ambazo huenda madhara yake usiyaone hivi sasa ila baadae utayaona.

Watafiti na Maafisa kilimo watafanya mpango wa kuwaelekeza wakulima baada ya kupata mbegu wawaeleze kinagaubaga juu ya ardhi ya sehemu husika kuwa inakubali zao gani na namna gani waweze kufanya kilimo chao.

Lakini pia serikali ifanye ufuatiliaji baada ya mwaka wa kwanza kupita katika majaribio yao waone wapi walikosea au wapi walipatia waboreshe. Hii ingeweza kuwafanikisha wakulima kupata kilimo cha maendeleo.

Serikali itoe pembejeo za kilimo mfano Treka, Mbolea na vifaa vingine ili kilimo kiwe cha haraka na walime eneo kubwa ambalo litaweza kuleta tija na faida miongoni mwao.

Baada ya kufanya ufuatiliaji wote huo bado watakuwa na kazi ya kufuatilia masoko ambayo yatawafanya wakulima wakitoka shambani basi wahifadhi chakula cha kutosha kujikinga na baa la njaa lakini pia wapate kuuza mazao yao kwa bei itakayowanufaisha.

Serikali ikifanya hivi basi itakuwa imeleta chachu kwa wakulima katika kubadilisha maisha yao ya kutoka katika ukulima wa kawaida hadi kufikia kilimo chenye tija na maendeleo na hapo watakuwa wamefanya tukio muhimu la kuwasaidia wakulima wao.

Kuna mazao ya kimkakati na kibiashara mfano Alizeti ambalo linalimwa sana kanda ya kati maarufu zaidi katika mkoa wa Singida. Lakini pia kuna zao la Kahawa , Karafuu na mazao mengine.
WAKULIMA, hawa ndio watendaji wa kazi bila ya hawa basi hakuna habari za kilimo ndio ambao wanalisha Watanzania kwa kiasi kikubwa sasa vipi hao wenyewe watajiweka sawa , mosi wanatakiwa wasikae kimya pale wanapoona wanahitaji msaada kutoka serikalini, pili wenyewe wanatakiwa wajitambue na wafahamu kuwa kilimo wanachokifanya kinatakiwa kilete tija na maendeleo yao wenyewe katika maisha ya kila siku.

Kuchagua eneo ambalo litaweza kusaidia kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija katika familia zao, kipi kilimo chenye tija ni kile ambacho kitaleta chakula cha kutosha hadi msimu unaokuja lakini pia wapate kiasi kidogo cha kuuza kwa ajiri ya matumizi yao ya kila siku.

Lakini pia waangalie na kusikiliza vyombo vya habari hasa habari kutoka Hali ya hewa ambayo itawasaidia kuwa msimu husika una mvua kiasi gani kwa ajairi ya mazao yao.

Msimu huu umekuwa wa hasara kutokana na hali ya hewa kuwa mbovu je wakulima hawafikiriii kuwa na chanzo mbadala katika kilimo chao, basi wanatakiwa wawekeze katika kilimo cha umwagiliaji ili kusiwe na mwanya endapo mvua isiponyesha au isiponyesha kwa kiasi ambacho kimetarajiwa.

Lakini pia wakulima waangalie namna gani wataweza kuhmili wadudu waharibifu kwa ajiri ya kukuza vyema mazao yao kwakuwa ndio hazina yao katika maendeleo ambayo wanayahitaji kuelekea katiia nchi ya ahadi.

Mkulima asipende kuuza mazao yake akiwa shambani kutokana na mabosi wegine huwa wanafika katika shamba na kutaka wanunue kabla hawavuna hii ni ishara ya umaskini vuna mazao yako kisha ndio uwe ana uhakika kama umepata kiasi gani ya kuuza tena kwa bei unayoitaka vinginevyo utakuwa umepoteza kitu kikubwa kama utauza mazao yakiwa shambani kwa nguvu kazi zako ulizotumia.

WAFANYABIASHARA, hawa nao wanasehemu yao nilinza kuwaelezea kidogo kuna muda wanakuwa wajanja wakitaka kununua mazao yakiwa shambani ili wawanyonye wakulima sasa hii haijakaa sawa wanatakiwa watende haki na waangalie pia namna gani wanapata faida lakini wasifikirie kupata faida mara mbili zaidi ya vile ambavyo wakulima wanapata.

Wafanyabiashara wengi wanapenda kuwanyonya wakulima wanatakiwa wafahamu kuwa katika swlaa la maendeleo wanatakiwa waendelee wotew faida yao isiwe zaidi ya kile alichochukua japo kwa wachumi wanahitaji faida zaidi.

Waandae bei itakayoweza kuwafurahisha wakulima kwakuwa bei nzuri itawafaidisha wakulima katika kutumia jasho lao ambalo wamelifanyia kazi kwa msimu mzima.

Kwa pamoja wote wakifanya hivi watakuwa wamefika katika hatua nzuri ya maendeleo na kulifanya taifa letu kufika mahali pazuri katika kugawana keki ya taifa.

Hakuna mkulima anayependa apate baa la njaa lakini pia hakuna mfanyabiashara asiyependa apate hasara lakini mkulima hapo ndio mfalme zaidi wa kutuliza akili yake na kuacha njaa isiyokuwa na msingi katka kuyaendea maendeleo yake mwenyewe.

Mwisho​
 
Upvote 0
Back
Top Bottom