Mkurugenzi wa Chadema Mh John Mrema amesema Chama chake kikifanikiwa Kupata Ushindi wa Kitongoji hata kimoja tu utakuwa ni Ushindi wa kishindo wa 100%
Mrema amesema 2019 Chadema haikushinda Kitongoji Kijiji wala Mtaa hata Mmoja hivyo Ushindi wowote Mwaka huu utakuwa ni 100%
Mrema amewaambia waandishi wa habari kwamba Chadema haina msamiati wa kujitoa Kwenye Uchaguzi huu
Ahsanteni Sana 😃
Hawa jamaa ni wapumbavu sana.
Hakuna chama cha siasa duniani kinachotegemea huruma ya watawala kitakacho shinda kwenye tawala za kiimla kama kinaongozwa na wala rushwa na mafisadi kama Mbowe.
Mbowe ameshakata tamaa baada ya kuona kuwa haungwi mkono na wananchi wote.
Kutoka peke yake kwenye maandamano ni ishara ya kuchokwa na jamii nzima. Mtu anayependa na watu wa chini hata akiwa gerezani watu wataandamana kwa ajili yake.
Mbowe alikaa gerezani zaidi ya miezi mitano lakini hakuna mtu aliyeandamana.
Mbowe akavunjwa mguu ,hakuna aliyeandamana.
Mbowe akaitisha mandamano hakuna aliyetoka.
Kifupi Mbowe hana wananchi wenye uchungu nyuma yake .
Hata Yesu alipokamatwa Mwanafunzi wake mmoja akishika upanga na kumkata mtu sikio kuonyesha hasira zake kwa waonevu.
Mbowe tangu alipotoka Mtu wa watu na mzalendo Dr. Slaa mpaka leo hakuna mwananchi anayeweza hata kurusha jiwe kumpigania zaidi ya familia yake mwenyewe .
Cha ajabu bado Mbowe halioni hilo kuwa ni ishara tosha ya yeye kuachia ngazi kabla ya ACT Wazalendo haijaanza kuwachukua Makada wa Chadema waliochoka kuona mkwamo mkubwa wa kisiasa ndani ya chadema .
Hivi kwa mfano mtu kama Makonda akiitisha maandamano atakosa wetu ?
Siasa za Tanzania zinataka mtu anayepamabana na mafisadi na kutetea wanyonge amaboa ndio wanaoandamana na kufunga barabara hata kuuawa . Mbowe amejikuta kwa matajiri ,na mafisadi huku akitumia chama kama sacoss ya kujipatia fedha