Chadema acheni ukorofi na ukaidi, heshimuni sheria na taratibu zilizowekwa

Chadema acheni ukorofi na ukaidi, heshimuni sheria na taratibu zilizowekwa

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Kuna kila dalili Chadema sasa wameanza chokochoko, mifano ipo mingi.

Mfano tukio lililo tokea mkoani Mwanza, viongozi kutoa matangazo kwa wanachi kuhudhuria mkutano wa ndani ambao haukufuata taratibu, hilo sio sahihi.

Chadema acheni ukorofi na ukaidi, heshimuni sheria na taratibu zilizowekwa.

Kwa jinsi mnavyoenda msije mkawalaumu polisi.
 
Kwamba?

"... viongozi kutoa matangazo kwa wanachi kuhudhuria mkutano wa ndani ambao haukufuata taratibu, .."

Weka hapa utaratibu wa kufuata kufanya mikutano ya ndani.
 
Lwaitama na wenzake wame amua kuichokoza na kuikejeli Serikali ya awamu ya 6.

Lwaitama kipindi cha Hayati JPM alikuwa kimya kama kamwagiwa maji sasa ameanza tena kufurukuta, aliufyata yeye na wenzake sasa naona wanataka kumjaribu Mama.

sasa nn kilimnyamazisha? na sasa nn kimemfanya aanze chokochoko na kejeli?
 
Tuongee ukweli lkni Hata hiko kibali cha mikutano mkiwaambia waifuate Korea kaskazini wakirudi nayo mtaikataa 😂😂
 
huyu inabidi atenguliwe kiuno, ili ajifunze kutofautisha itikadi na taaluma.
kapoteza kabisa sifa ya kuitwa msomi.

nilisikiza clip yake moja akihutubia, nilisikitika sana! msomi mzima anaongea kejeli na kebehi badala ya kujenga hoja zenye mashiko!!
ndugu Lwaitama unawaaibisha wasomi wa chuo kikuu, badilika mzee, huwezi kupata sifa kwa kulopoka zaidi ya kudhalilisha usomi wako, bora uige mfano wa prof. hayati Baregu.
 
Tunavitaka vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kamwe visikubali au kuachia amani yetu ikichezewa na watu wachache. kamwe tusiziachie hizi chokochoko ziendelee, lazima nchi yetu itulie kama ilivyo kuwa kipindi cha hayato JPM ndipo maendeleo yatapatikana.
 
Hapo Kuna anaevunja taratibu na anaevunja katiba,Cha msingi tumeona madhara ya kujazwa wanachama wa chama kimoja bungeni kila kitu kinapitishwa enzi za akina lissu ,msigwa ,sugu,heche,hilima mdee,siyo mdee huyu wa Sasa,pasingepitishwa kitu hapo,,na sisitiza tukatwe makato ndiyo Ila chooonde zikanye Mambo mazuri,na kwanzia Leo habari za sherehe sherehe zifutwe,taifa bado changa Sana kusherehekea
 
Amiri Jeshi Mkuu kasema kwa sasa hawezi kuruhusu mchakato wa katiba mpya, tumpe muda lkn viongozi wa chadema wamekosa ustaarabu wameamua kukaidi amri halali sasa naona ni vyema sheria ichukua mkondo wake.
 
Back
Top Bottom