Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Bila kuwa mwanachama wa Chadema au ACT Wazalendo, nakiri kwamba Chadema, hawa kina Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Mbowe, na wakati fulani kina Msigwa, Dr. Slaa, Mtikila, Mrema, Dr. Kaborou na wengine, siku zote wamekuwa na nia nzuri sana na nchi yetu. Sina shaka juu ya hilo.
Sasa tatizo ni kwamba kwa upande mmoja, wanakabiliana na CCM ambayo iko tayari kutumia mbinu yeyote ile kubakia madarakani, hata kama mbinu hiyo ni kumnyima mtu haki ya kuishi. CCM imejizatiti mno katika kubaki madarakani, na sioni hata siku moja kwamba CCM wanaweza kuondolewa madarakani kwa njia ya kura katika uchaguzi halali. Labda waondoke kwa mapinduzi ya kutumia nguvu.
Kwa upande wa pili, tatizo lipo kwa Watanzania. Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo mwamko wa kisiasa uko kiwango cha chini huenda kuliko nchi zote duniani. Tanzania ina wananchi wengi ambao hawana uwezo wa kisiasa wa kufikiri ili kuamua mambo kuhusu maisha yao wenyewe. Leo hii, ukimweka mtu toka gerezani alifungwa kwa kosa la wizi na ubakaji akawa mgombea wa CCM, Chadema au ACT Wazalendo, huenda hata waliobakwa ni ndugu wa wafuasi wa vyama hivyo, bado watamshangilia na kumpigia kura! Kwa kifupi, Watanzania wengi ni "political illiterates" na "blind supporters" wa kiasiasa. Sera za chama, uwezo wa kuongoza, uadilifu na utendaji wa nyuma wa wagombea uongozi kwao sio jambo kuu, bali chama chao ndio jambo kuu.
Sasa basi, kina Mbowe, Zitto, Lissu, wafanyeje ili kutimiza azma yao nzuri ya kuiokoa nchi hii?
Nawashauri kuwa watumie kanuni ambayo imedhihirika kwa muda mrefu sana - if you cant beat them, join them. Ifikie mahali hawa kina Chadema wakubali kwamba hawawezi kuipigania nchi hii toka nje ya CCM, bali inabidi wawe shemu ya CCM. Wakubali kuingia ndani ya CCM kama walivyofanya kina Msigwa, Prof. Kitila, Kafulila, nk. Hawa watu nina uhakika watatoa mchango ndani ya CCM kuliko walivyowahi kufanya katika maisha yao yote ya kuwa kwenye vyama vya upinzani. Labda tunapaswa tuanze kumfikiria Mbowe kama Waziri Mkuu, Lissu kama waziri wa sheria, Zitto kama waziri wa fedha na uchumi, Lema kama waziri wa mambo ya ndani, nk. Kama hili haliwezekani katika serikali ya mseto, basi hawa watu waingie CCM ili tuijenge Tanzania pamoja, bila kugombana kila siku
Najua CCM wakiona leo Tundu Lissu au Mbowe nk wanataka kuingia CCM watashituka. Basi inabidi kufanya kila namna kwamba hili lifanyike. Ikibidi, turudie referandum ya kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Jambo moja tunakiri, huu mfumo wa vyama vingi hautusaidii kwa lolote. Lengo lilikuwa zuri sana, lakini tatizo ni kwamba CCM wametumia nafasi waliyonayo kuwa wabinafsi sana kiasi kwamba ile nia nzuri ya kuwa na vyama vingi haipo tena. Kila siku inayopita mfumo wa vyama vingi unazidi kukuza uadui kati ya watanzania, umezorotesha muungano wa bara na visiwani, na unapandikiza mbegu za chuki hata ndani ya familia moja moja!
Kama hili haliwezekani, basi mie bila uoga wala kuficha, ninatoa wito kwa jeshi letu la wananchi, JWTZ, kuchukua hatamu za uongozi kwa muda kama miaka miwili hivi katika utaratibu unaokubalika pamoja na AU, SADC na EAC, ili tujipange upya, kwa kufuta vyama vyote vya siasa vilivyopo na kuanzisha vyama vipya kabisa na kutengeneza uwanja sawa wa ushindani wa kiasiasa, kisha uchaguzi mkuu uitishwe.