CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Kuna hizi ahadi CHADEMA mliahidi:
1. Mliahidi mtateua watendaji wenu serikali za mitaa ili watoe huduma kwa wananchi kwa kuwa hamuwatambui waliochaguliwa uchaguzi mdogo. Mmefikia wapi? Wanatoa huduma gani? Tupeni majina ya viongozi wenu tuwape kero zetu.
2. Mlidai kupitia zoezi la chadema ni msingi mumepata wanachama milioni 10. Mnayo orodha? Mshampa msajili?
3. Mliahidi mtachapisha orodha ya waliochangia viongozi watoke jela na ina mpaka mama lishe. Kaka Makene orodha tayari? Nataka nione jina la mama lishe wa pale Rombo Usseri. Kama bado tunakukumbusha inasubiriwa. Au michango ilizidi mlichotangaza maana nyie mhh!
4. Nikumbushe tena ahadi yenu ya kuunda CHADEMA CORONA TASK FORCE ya kukusanya majina ya wafu. Mmefikia wapi? Kina nani wanahesabu maiti? Mpaka sasa Corona imeua wangapi? Ningependa kujua idadi ya wamachame waliokufa kwa corona tafadhali.
5. Zile ahadi za kuwasusia RC wa Dar na DC wa Hai mmetekeleza kwa kiwango gani? Nini mmeshawasusia?
6. Ahadi za kusaidia familia za wafiwa mfano Mawazo na Mwangosyi mnatekeleza au wajihudumie wenyewe?
Hivi mnapotoa ahadi sampuli hii mnakuwa mmeshauriana au mtu mmoja anaagiza mtangaze hizi ahadi?