mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Waliokuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti na wajumbe kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Ungalimited jijini Arusha wamelalamikia rufaa zao kutokusikilizwa na kutupiliwa mbali na hiyo ni baada ya kuenguliwa kwa majina ya wenyeviti na wajumbe kwa asilimia 90% huku likipitishwa jina la mwenyekiti mmoja tu wa chama hicho
Wakizungumza hii leo Novemba 20, 2024 baadhi ya wagombea hao akiwemo mjumbe wa Baraza la Wazee wa Chama hicho kata ya Ungalimited Bi Asia Muhammad amemuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kurudishwa kwa wagombea walioenguliwa majina yao ili kudhihirisha uwepo wa demokrasia katika nchi na sio chama kimoja kupendelewa.