kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeipongeza serikali kwa kuanza kuboresha mazingira ya haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kutoa maoni. Hayo yalisemwa na Chama hiko wakati wa maadhimisho ya siku ya haki za binadamu kupitia Tamko la kimataifa la Haki za kibinadamu (UDHR) ambayo hufanyika Desemba 10.
Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa wa CHADEMA, Mch Peter Msigwa, alibainisha kuanza kuimarika kwa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni alipozungumza wakati wa kongamano hilo lililofanyika mjini Iringa. Alisema Serikali duniani kote ina wajibu wa kuhakikisha inalinda haki za raia wake, ikiwemo haki ya kuishi, kukusanyika, kutoa maoni na nyinginezo.
Mch Msigwa alisema hali ya kujieleza hapo nyuma ilikuwa siyo ya kuridhishwa lakini kwa sasa mambo yameanza kubadilika katika ki[indi hiki cha Serikali ya awamu ya sita.